logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watu 3 wameaga dunia kufuatia ajali ya barabara Machakos

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Matungulu Monica Kimani alithibitisha kisa hicho.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri21 December 2021 - 14:34

Muhtasari


  • Watu 3 wameaga dunia kufuatia ajali ya barabara Machakos
  • Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Matungulu Monica Kimani alithibitisha kisa hicho

HABARI NA GEORGE OWITI;

Watu watatu wamefariki huku wengine kadhaa wakipata majeraha katika ajali mbaya katika barabara ya Koma - Kenol kaunti ya Machakos.

Meneja wa Hospitali ya Kangundo Level 4, Evayo Loveto alisema miili tatu, miwili ya wanawake na mmoja wa mtoto imehifadihiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo.

Walioshuhudia walisema watatu hao walikufa papo hapo baada ya gari lao aina ya probox kugongana  ana kwa ana na prado kati ya Koma Hill na Kenol karibu na soko la Masokani katika Kaunti Ndogo ya Matungulu siku ya Jumanne.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Matungulu Monica Kimani alithibitisha kisa hicho.

Kimani, hata hivyo, alisema bado hajapata maelezo ya ajali hiyo kutoka kwa maafisa wake ambao alisema walikuwa bado wanatoka kuwahudumia waathiriwa.

"Hakuna maelezo bado, maafisa bado wako nje," Kimani aliambia Star.

Mabaki ya magari hayo mawili yalivutwa hadi kituo cha polisi cha KBC yakisubiri ukaguzi.

 

 

 

 

 

 

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved