logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamke anayeshukiwa kumuua jirani azuiliwa kwa siku 8

Hakimu mkazi mkuu wa Milimani Jane Kamau alimzuilia Clementine Nandutu katika kituo cha polisi cha Gigiri

image
na

Habari03 January 2022 - 13:38

Muhtasari


  • Hakimu mkazi mkuu wa Milimani Jane Kamau alimzuilia Clementine Nandutu katika kituo cha polisi cha Gigiri

Mwanamke anayeshukiwa kusababisha kifo cha jirani yake baada ya kisa cha mapigano katika kitongoji duni cha Kabarage huko Kangemi, Nairobi, amezuiliwa kwa siku nane akisubiri uchunguzi.

Hakimu mkazi mkuu wa Milimani Jane Kamau alimzuilia Clementine Nandutu katika kituo cha polisi cha Gigiri baada ya kufanikiwa ombi la polisi.

Katika hati ya kiapo iliyowasilishwa mahakamani na afisa mchunguzi Charles Muchoya, alitaka siku 14 kukamilisha uchunguzi akisema ni kosa kubwa.

Mahakama iliarifiwa kwamba Nandutu ni mkazi wa kitongoji duni cha Kibarage ambako marehemu Mary Njambi pia aliishi na iwapo ataachiliwa, anaweza kuingilia upelelezi.

"Mshukiwa alipigana na marehemu mnamo Desemba 27 mwaka jana na hivyo kusababisha majeraha yake ya mwili yanayoshukiwa kusababisha kifo chake mnamo Januari 1, 2022", afisa huyo aliiambia mahakama.

Muchoya aliendelea kusema kuwa marehemu alifariki katika nyumba ya mamake.

Afisa huyo anataka kumfanyia uchunguzi wa kiakili mshukiwa huyo na kupata ripoti ya uchunguzi wa kifo cha marehemu ili kubaini chanzo cha kifo hicho.

Simu ya mshukiwa na ya marehemu bado hazijawasilishwa kwa uchunguzi wa kitaalamu.

Nandutu alijitetea dhidi ya kuzuiliwa na kuiambia mahakama kuwa hana hatia na kwamba polisi wanafanya uovu kwa kutaka azuiliwe.

Hakimu, hata hivyo, alisema siku 14 zilizoombwa zitakuwa ndefu sana na zitapewa siku nane pekee. Kesi itatajwa Januari 12.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved