logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Carabao Cup: Arsenal vs Liverpool yaahirishwa, Chelsea yatamba nyumbani

Mapema wiki hii Liverpool iliomba mechi ya mkondo wa kwanza ugani Emirates iahirishwe kutokana na ongezeko la visa vya COVID-19 katika kambi yao.

image
na Radio Jambo

Habari06 January 2022 - 04:13

Muhtasari


•Mapema wiki hii Liverpool iliomba mechi ya mkondo wa kwanza ugani Emirates iahirishwe kutokana na ongezeko la visa vya COVID-19 katika kambi yao.

•Kai Havertz alifungia Chelsea bao la kwanza katika dakika ya tano huku mlinzi Ben Davies wa Spurs akiingiza mpira katika lango lake takriban nusu saa baadae.

Mchezaji wa Arsenal Takehiro Tomiyasu (kulia) amelala kwa huzuni baada ya kipenga cha muda wote dhidi ya Manchester City.

Ligi ya Soka ya Uingereza (EFL) imeafikia kuahirihisha mechi ya nusu fainali ya Carabao kati ya Arsenal na Liverpool ambayo ilitarajiwa kuchezwa usiku wa Alhamisi.

Hii inafuatia ombi la Liverpool mapema wiki hii la kutaka mechi ya mkondo wa kwanza ugani Emirates iahirishwe kutokana na ongezeko la visa vya COVID-19 katika kambi yao.

Siku ya Jumatano EFL ilikubali ombi la Liverpool na  kusukuma mechi hiyo hadi Alhamisi, Januari 20.

Kufuatia hayo ratiba ya nusu fainali ya Carabao Cup kati ya timu hizo imebadilishwa na sasa raundi ya kwanza itachezwa ugani Anfield mnamo Januari 13.

Arsenal imewaomba mashabiki wake radhi kwa hiilafu iliyoababishwa huku ikiwahakikishia kuwa tiketi ambazo walikuwa wamenunua bado zitakuwa halali tarehe mpya iliyowekwa.

Liverpool kwa upande mwingine imeshukuru EFL na Arsenal kwa kuelewa jinsi hali ilivyo katika kambi yao.

Kwingineko Chelsea na Tottenham walikutana usiku wa Jumanne ugani Stamford Bridge  katika raundi ya kwanza ya semifainali ya kombe la Carabao.

The Blues waliwika nyumbani na kuwaangamiza majirani wao Spurs kwa mabao mawili kwa sufuri katika mechi hiyo iliyochezwa mwendo wa saa tano kasorobo.

Kai Havertz alifungia Chelsea bao la kwanza katika dakika ya tano huku mlinzi Ben Davies wa Spurs akiingiza mpira katika lango lake takriban nusu saa baadae.

Raundi ya pili ya semifainali kati ya timu hizo mbili za London itachezwa mnamo Januari 12. 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved