logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pombe iliyotengezwa kutumia ndizi yasababisha vifo vya watu 11

Watu wanne zaidi wanaripotiwa kuwa hospitalini kwa matibabu lakini tayari wamepofuka.

image
na Radio Jambo

Habari06 January 2022 - 04:09

Muhtasari


•Watu wanne zaidi wanaripotiwa kuwa hospitalini kwa matibabu lakini tayari wamepofuka.

Watu 11 wameripotiwa kufariki nchini Rwanda tangu siku kuu ya Krismasi baada ya kunywa pombe ya kienyeji inayotengezwa kutumia ndizi katika wilaya ya kusini mashariki mwa nchi hiyo ya Bugesera.

Watu wanne zaidi wanaripotiwa kuwa hospitalini kwa matibabu lakini tayari wamepofuka.

Watu watano walikamatwa siku ya Jumatatu kuhusiana na tukio hilo, akiwemo mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe hiyo nchini humo, Ofisi ya Upelelezi ya Rwanda imethibitisha.

Viwango vya juu vya methanoli vilivyopatikana katika moja ya bia hiyo kwa jina Umuneza, vinaweza kuhusishwa na vifo hivyo, kulingana na Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Rwanda.

Kiwanda cha bia kinachojulikana kama Rwandabev kilikuwa kikifanya kazi bila leseni.

Kampeni ya nchi nzima imezinduliwa ili kubana pombe za kienyeji ambazo hazijaidhinishwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved