logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DPP Haji aagiza uchunguzi ufanyike kuhusu matamshi ya Seneta Linturi katika mkutano wa Ruto Eldoret

Kulingana na DPP, matamshi ya Linturi yanaweza kuchochea dharau, chuki, uhasama, vurugu au ubaguzi.

image
na Radio Jambo

Habari08 January 2022 - 20:35

Muhtasari


  • DPP Haji aagiza uchunguzi ufanyike kuhusu matamshi ya Seneta Linturi katika mkutano wa Ruto Eldoret
  • Kulingana na DPP, matamshi ya Linturi yanaweza kuchochea dharau, chuki, uhasama, vurugu au ubaguzi
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Noordin Haji ameagiza uchunguzi ufanyike kuhusu matamshi ya Seneta wa Meru, Mithika Linturi mjini Eldoret wakati wa mkutano wa Naibu Rais William Ruto.

Katika barua kwa Inspekta Jenerali, Hillary Mutyambai, Haji alimwagiza afungue uchunguzi kuhusu matamshi ya seneta huyo.

Kupitia kwenye video iliyosambaa mitandaoni Linturi alisema;

Sisi tunataka kuwa kwa serikali inayokuja lakini nawaambia watu wa Uasin Gishu msicheze na Kenya na kile nawaomba ni kwamba madoadoa yale mliyonayo hapa muweze kuondoa. Hatuwezi kuwa tukisimama na William Ruto kule Mt Kenya na mko na wengine hapa hawasikii na hawawezi ungana naye..."

Kulingana na DPP, matamshi ya Linturi yanaweza kuchochea dharau, chuki, uhasama, vurugu au ubaguzi.

"Kwa mujibu wa Kifungu cha 157 (4) cha Katiba, ninaagiza kwamba ufanye uchunguzi wa kina mara moja kuhusu madai hayo na uwasilishe faili ya uchunguzi wa matokeo kabla ya tarehe 14 Januari, 2022," Haji alisema.

Matamshi yake yalikasirisha Wakenya kwenye Twitter wakiwemo viongozi ambao wamejitokeza kukashifu vikali matamshi ya seneta huyo wa Meru.

Moses Kuria alikashifu matamshi hayo akisema kuwa Naibu Rais William Ruto alifaa kukemea matamshi ya Linturi.

"Mimi ni rafiki wa karibu wa Naibu Rais. Hata hivyo niko mbali. Ikiwa uko Eldoret na karibu sikia mwambie akemee mazungumzo haya. Haijalishi iwe inasemwa na Linturi au Oscar Sudi. Ni muhimu kwamba inasemwa huko Eldoret Sports Club, kilomita chache kutoka Kanisa la KAG Kiambaa katika Msitu wa 'Burnt' Jameni Madoadoa tena," Kuria alisema.

Viongozi wengine pia walilaani matamshi hayo;

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved