logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Kuwa mwangalifu!" King Kaka atuma ujumbe kwa daktari aliyempima vibaya na kumsababishia ugonjwa

King Kaka amesema kwamba hana kinyongo chochote dhidi ya daktari mhusika.

image
na Radio Jambo

Habari14 January 2022 - 07:46

Muhtasari


•Baba huyo wa watoto watatu alifichua kwamba tayari amerejesha uzito mkubwa mwilini baada ya kuwa amepoteza zaidi ya kilo 33 alipokuwa mgonjwa.

•Mwanamuziki huyo alisema wakati alipokuwa mgonjwa alikuwa amelemewa kiasi cha kwamba tayari alikuwa ameandika wosia iwapo ingetokea ashindwe kupambana na ugonjwa.

•King Kaka amesema kwamba hana kinyongo chochote dhidi ya daktari mhusika.

Mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za kufoka Kennedy Ombima almaarufu kama King Kaka amezungumza kuhusu jinsi anavyoendelea baada ya kukabiliwa na ugonjwa wa kutisha kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu mwaka jana.

Akiwa kwenye mazungumzo na Mwafrika katika kipindi cha 'Iko nini', mwanamuziki huyo alisema kwa amepata nafuu kikamilifu na tayari hisia yake ya ladha na hamu ya chakula imerejea.

Baba huyo wa watoto watatu alifichua kwamba tayari amerejesha uzito mkubwa mwilini baada ya kuwa amepoteza zaidi ya kilo 33 alipokuwa mgonjwa.

"Ugonjwa iliisha. Nashukuru Mungu, saa hii niko na hisia ya ladha na nakula. Kuna wakati nilianza kula, nilipatiwa madawa ya kunisaidia kurejesha hamu ya chakula. Saa hii niko na kilo 78. Nilikuwa nimepungua hadi kilo 60, saa hii nimeongeza kilo 18. Daktari alisema nimeongeza uzito haraka sana" King Kaka alisema.

Rapa huyo amesisitiza kwamba ugonjwa wake ulisababishwa na  madawa aliyopatiwa kufuatia utambuzi mbaya wa daktari.

Licha ya madhara ambayo utambuzi huo mbaya ulimsababishia mwilini, King Kaka amesema kwamba hana kinyongo chochote dhidi ya daktari mhusika. Hata hivyo amemshauri daktari huyo kumakinika zaidi katika kazi yake.

"Hatujawahi kuzungumza na daktari huyo. Mimi ni mtu wa kusameheana sana. Nilindokea  tu, maisha huwa hivo. Hakufanya akitaka. Nina uhakika ametazama mahojiano mengi ambayo nimefanya, mahali yuko tu awe tu mwangalifu, pamoja na madaktari wengine wote" Alisema King Kaka.

Mwanamuziki huyo alisema wakati alipokuwa mgonjwa alikuwa amelemewa kiasi cha kwamba tayari alikuwa ameandika wosia iwapo ingetokea ashindwe kupambana na ugonjwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved