Aliyekuwa rais wa Amerika Barack Obama siku ya Jumatatu alitumia ukurusa wake wa Twitter kuchapisha ujumbe kwa mkewe akimtaja kuwa mwendani wake na mpenzi wa karibu.
Michelle alikuwa anasherekea siku ya kuzaliwa kwa kufikisha miaka 58.
Baba huyo wa watoto wawili aliwaeleza wafuasi wake kwamba Michelle si tu mke wake bali rafiki wake wa kufa kuzikana.
"Heri njema ya kuzaliwa, Michelle. Mpenzi wangu,mshirika wangu...rafiki yangu mkubwa ...
Michelle katika picha iliyochapishwa na rais huyo wa zamani wa Marekani, alionekana akimpiga busu mpenzi wake huku wote wakitabasamu na kupendeza pamoja, Michelle akiwa na kinywaji mkononi.
Vile vile, mashabiki walimtakia Michelle heri njema ya kuzaliwa kupitia sehemu ya maoni ya ukurasa wa Obama.
