logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Yamoto Band kuzinduliwa upya, meneja atangaza

Mkubwa Fella kupitia kituo kimoja cha radio nchini Tanzania ametangaza rasmi kuwa kikundi hicho mwaka huu 2022 kinarudi kuwapa burudani mashabiki wake

image
na

Habari19 January 2022 - 05:29

Muhtasari


• Yamoto band kimetangaza kurejea kwa kishindo kikubwa, hii ni  baada ya kusambaratika kwake.

•Amesema amesajili wasanii wapya ambao wataleta mhemko wa aina yake na kuzuzua nyoyo za mashabiki wa Bongo.

• ametangaza rasmi kuwa kikundi hicho mwaka huu 2022 kinarudi kuwapa burudani mashabiki wake.

Mkubwa Fella

Kikundi cha wanamuziki kutoka nchi ya Tanzania  cha Yamoto band kimetangaza kurejea kwa kishindo kikubwa baada ya kusambaratika miaka kadhaa iliyopita.

Mkubwa Fella kupitia kituo kimoja cha radio nchini Tanzania ametangaza rasmi kuwa kikundi hicho mwaka huu 2022 kinarudi kuwapa burudani mashabiki wake.

Kulingana naye bendi hio ilisambaratika kufuatia wanachama wake kuanza kurekodi muziki nje ya kikundi hicho,  jambo ambalo lilikuwa kinyume na mikataba yao.  

Wasanii walioanzisha kikundi hicho, walikuwa  Aslay, mbosso, Enock Bella na meneja akiwa Mkubwa Fella. 

Mkubwa Fella amesema mwaka 2022 anataka kuhakikisha kikundi hicho kimerudi  kwa kishindo na mashabiki wake watarajie muziki waliokosa wakati kikundi hicho kilingia mitini.

 Fella ambaye pia ni mbunge alisema  kwamba, ifikiapo mwezi wa Februari wataachilia kibao chao cha kwanza na hivyo kuomba mashibiki   kuwapokea kama kitambo.

Fella ambaye alijulikana kwa  ubunifu wake wakati bendi hiyo ilikuwa inatesa anga.  amesema amesajili wasanii wapya ambao wataleta mhemko wa aina yake na kuzuzua nyoyo za mashabiki wa Bongo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved