logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mchumba Hasomeshwi – Baba Levo amwambia Rayvanny

Baba Levo kupitia kituo kimoja cha runinga nchini Tanzania amedai kwamba alimuonya Ravyaan kutomlipia karo Kajala kwenda kusoma nchi za ng'ambo.

image
na

Habari26 January 2022 - 04:42

Muhtasari


  • Baba lebo kupitia kituo kimoja cha runinga nchini Tanzania amedai kwamba alimuonya Ravyaan kutomlipia karo Kajala kwenda kusoma nchi za ngambo.
  • Niseme moja kati ya vitu vimetrendi sana..ni Ravyaan na Mchumba wake Paula Kajala, naona kama taa nyekundu imewaka. Ravyaan aliniambia anamlipia ada.Mchumba hasomeshwi
Ravyaan

Siku ya Jumanne wiki hii  kumekuwa na tetesi kemkem ambazo zilisambaa kwa kasi kama moto wa karatasi kwenye ulingo wa burudani kwamba Rayvanny na Paula Kajala kaachana.

Baba Levo kupitia kituo kimoja cha runinga nchini Tanzania amedai kwamba alimuonya Ravyaan kutomlipia karo Kajala kwenda kusoma nchi za ng'ambo.

“Niseme moja kati ya vitu vimetrendi sana..ni Ravyaan na Mchumba wake Paula Kajala, naona kama taa nyekundu imewaka. Ravyaan aliniambia anamlipia ada .Mchumba hasomeshwi,” alisema Baba Levo.

Aliendelea kueleza kuwa, “Mabinti wengi wamezoea kula hela za watu halafu wanawakataa..hata kwa mabaha, ngumi nyingi hutokea kwa sababu hiyo,Mwanamke anaenda analewa pombe ya mtu kisha anatoroka,”

Alipoulizwa kwa nini  amesema hayo kuhusu mchumba  wa Rayvanny, alidokeza kwamba Ravyanny na kajala ni marafiki wakubwa kwenye mtandao wa kijamii.

“Wote ninawafuatilia kama jamaa zangu na marafiki zangu, nimeenda kwenye kurasa zao za mitandao wote wameacha kufuatiliana” alidokeza Baba Levo.Na kweli penye moshi hapakosi moto na tunachosubiria nikuona kama watazungumzia mahusiano yao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved