logo

NOW ON AIR

Listen in Live

CJ Koome awahakikishia maafisa wa mahakama usalama baada ya shambulio la Lamu

Koome aliagiza zaidi kwamba wahamishwe hadi Nairobi kwa uangalizi maalum zaidi.

image
na Radio Jambo

Habari27 January 2022 - 12:07

Muhtasari


  • CJ Koome awahakikishia maafisa wa mahakama usalama baada ya shambulio la Lamu

Jaji Mkuu Martha Koome amewahakikishia maafisa wa mahakama kote nchini usalama wao kufuatia shambulizi linaloshukiwa kuwa la al-Shabaab katika kaunti ya Lamu siku ya Jumatano.

Timu ya maafisa wa mahakama walipigwa risasi Jumatano na kujeruhiwa na watu wenye silaha walipokuwa wakielekea katika mji wa Garsen kutoka Mahakama ya Rufaa ya Kipini mwendo wa saa 5.50 usiku.

Walishambuliwa Lango la Simba, Kaunti ya Lamu.

CJ Koome alisema ameagiza Kitengo cha Polisi cha Mahakama kuchunguza hali ya usalama ya majaji, maafisa wa mahakama na wafanyakazi na kuchukua hatua zinazofaa ili kuhakikisha usalama wao.

"Ningependa kuwahakikishia majaji wenzangu, maafisa wa mahakama na wafanyakazi kwamba mahakama inathamini usalama wa watu na washirika wetu wote wanaofanya kazi katika mazingira magumu sana ili kupata haki.

Upatikanaji wa Haki kwa Wakenya wote," Koome alisema kwenye taarifa yake.

Alithibitisha kuwa waliojeruhiwa katika shambulio hilo ni Hakimu Mkuu Mwandamizi Mhe. Paul Rotich, karani wa Mahakama Boy Njue, Frank Sirima (ODPP) Konstebo wa Polisi Moses Bett na Willis Mgendi pamoja na dereva wao Abel Barisa.

Koome aliagiza zaidi kwamba wahamishwe hadi Nairobi kwa uangalizi maalum zaidi.

CJ alimsifu inspekta jenerali wa polisi Hillary Mutyambai kwa hatua ya haraka iliyochukuliwa na afisa wake katika kukamata shambulizi lililowaacha maafisa wake kujeruhiwa.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved