logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamume niko naye akiniacha nitarudi kwako asiponiacha potea-Mwanamke amkataa mumewe hadharani

sijawahi muona mwanamume anamlilia mwanamke ilhali amemkataa uliniambia una wanawake wa kutosha

image
na Radio Jambo

Habari27 January 2022 - 05:49

Muhtasari


  • Bwana Stephen alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe ambaye walikosana naye kwa ajili ya vitina kutoka kwa familia

Bwana Stephen alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe ambaye walikosana naye kwa ajili ya vitina kutoka kwa familia.

"Naomba nipatanishwe na mke wangu ambaye tulikosana naye kutokana na vitina kutoka kwa mashemeji na familia, ambao walisema kwamba nilikuwa naenda nje ya ndoa na kuniacha,"Stephen Alieleza.

Huku baada ya kumfikia mkewe alisema kuwa;

"Mimi nishaaolewa na nimekwambia uendelee na maisha yako, nikiwa naye alikuwa anaenda nje ya ndoa na kuniambia kwamba anaweza fanya ngono na mwanamke mwingine na kuniacha

Alinitesa katika ndoa, ambapo walinitusi wakisema kwamba siwezi pata ujauzito, na sasa nimepata, nikimwambia twende kwa daktari nilikuwa naenda pekeyangu alinifukuza na kuniambia nitoke niende kwamba kuna mwanamke mwingine anapaswa kuwa kwa nyumba yake

Alimpa mke wa bosi yake mimba, sijawahi muona mwanamume anamlilia mwanamke ilhali amemkataa uliniambia una wanawake wa kutosha

Huyu mwanamume niko naye akiniacha nitarudi kwako asipo niacha potea."

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved