Mwanasosholaiti na Muigizaji maarufu nchini Tanzania, Irene Uwoya ameeleza kwa nini huwa anapenda jinsia kiume kuliko ile ya kike.
Wiki jana muigizaji huyo kwenye eneo la burudani alionekana akigawa pesa kwa mashabiki wake, jambo ambalo lilifanya wanamtandao wabaki vinywa wazi walipoona video iliyokuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakishindwa mahali anatoa pesa zake.
Baada ya tetesi kwamba muigizaji huyo anatoka kimapenzi na wanaume wengi amesema sababu zake kuwa na uhusiano mzuri na wanaume.
Kupitia ukurusa wake wa Instagram amejitokeza na kueleza bayana kwamba uhusiano baina yake na wanawake huwa sio mzuri, kwa sababu jinsia ya kike watakufurahia usoni ila kwenye roho hawakuwa na furaha kutokana na mafanikio yako.
Alipongeza wanaume kwa sababu wao humwambia ukweli wakati wote na kuwapongeza kufurahia mafanikio yake.
"Watu wanauliza sina marafiki wa kike?kiukweli asilimia 90 ya marafiki zangu ni wanaume, sababu wamenyooka sana ukikosea wanakwambia na ukifanya vizuri wanakupongeza na ukifanikiwa wanaufurahia mafanikio yako kama Yao,ila wakike anakuchekea machoni moyoni anatamani ufe…simanishi siwapendi ila napenda tuonane kwa mbali" alisema Irene Uwoya.