Muigizaji na mjasirimali Minnie Kariuki alifahamika sana kupitia uigizaji wake katika kipindi cha Tabasamu kilichokuwa kinapeperushwa kwenye runinga ya Citizen.
Huku akizungumzia safari yake ya uigizaji, akiwa kwenye mahojiano, alisema kwamba alitaka kuwa wakili, ili kupigania haki za binadamu.
"Nikiwa shule ya upili nilitaka kuwa wakili, lakini nilijijua baada ya kutoka kidato cha nne kwani nilifanya vyema katika uigizaji
Katika uigizaji wa Tabasamu, niliigiza kwa miaka 4, nakumbuka tukipigiwa simu na kuambiwa Tabasamu imekamilika, nililia kwa sababu sikuwa na kazi nyingine
Nilipatwa na msongo wa mawazo kwa miezi 3, niliamua kuanza biashara na nilitamani kazi ya ujenzi," Aliongea Minnie.
Pia muigizaji huyo anaigiza katika kipindi cha Single-ish, na pia aiigiza katika kipindi cha 'My Empress' kilichokuwa kinapeperushwa kwenye runinga ya Maisha Magic East.
Kando na uigizaji wake Minnie ni mama na mke wa mtu, alisema kwamba hakuwa naataka kuandikwa ndio maana alianzisha biashara yake
Pia aliwshauri wanawake ambao wanawategemea wanaume, kuwa pesa za wanaume haziwezi kuwakimu maishani.
