logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kimemia: Viazi vya Nyandarua kupata soko KFC, Congo

Gvana wa Nyandarua Francis Kimemia amesema KFC imekubali mkataba wa kutumia vianzi vya nchini

image
na Radio Jambo

Habari11 February 2022 - 07:51

Muhtasari


• Gavana Francis Kimemia amefichua kwamba wamefikia makubaliano na wamiliki wa mgahawa wa KFC ili kutumia viazi vya wakulima hao kutengeneza vibanzi.

• Makubaliano hayo yanatarajiwa kung’oa nanga mwenzi Machi

Ni habari mpya tena ya kutia moyo kwa wakulima wa viazi kutoka kaunti ya Nyandarua baada ya gavana Francis Kimemia kufichua kwamba wamefikia makubaliano na wamiliki wa mgahawa wa KFC ili kutumia viazi vya wakulima hao kutengeneza vibanzi.

Katika mazungumzo na mtandao wa kidigitali wa runinga ya Citizen, Februari 10, gavana Kimemia alisema kwamba makubaliano hayo yaliafikiwa kwamba wakulima wa humu nchini wa zao hilo watakuwa wanasambaza Viazi sio tu kwa mgahawa wa KFC bali hadi kwa masoko ya kimataifa kama vile Congo na mengine.

Gavana huyo aliwataka wakulima waache kuwalaumu KFC kwa kuagiza viazi kutoka nje kwa sababu huo ni mgahawa mkubwa tena tajika si tu Kenya bali kote ulimwenguni na walikuwa wanafanya hivo kwa sababu ya ubora wa viazi viazi hivyo ambao haupo katika viazi vya humu nchini.

“Matawi mengi ya KFC wanataka viazi vya aina fulani ambavyo hapa Kenya hatuwezi tukavikuza lakini katika makubaliano tulikubaliana nao (KFC) kwamba tunaweza anza kukuza aina hiyo ya viazi ili kuafikia vigezo vya kiafya na ubora,” alisema Kimemia

Pia gavana Kimemia alisema kwamba walielewana na wakuu wa KFC kushirikiana na wakulima wa humu nchini ili kuwapa mafunzo jinsi ya kupanda na kukuza aina hiyo ya viazi

Makubaliano hayo yanatarajiwa kung’oa nanga mwenzi Machi na gavanac Kimemia alisema hili litakuza soko la viazi nchini Kenya na kote ulimwenguni.

“Tutaanza kupanda viazi hivyo mwezi Machi na tunategemea kufikia mwezi Juni tutakuwa tunasambaza zao letu la kwanza kwenye masoko nac kuanzia hapo tutaongeza,” alisema Kimemia

Mgahawa wa KFC uligonga vichwa vya habari mwishoni mwa mwaka jana walipotangaza kuwa wana uhaba wa viazi vya kupika vibanzi na kusema kwamba hawawezi tumia viazi vya humu nchini kutengeneza vibanzi katika matawi yao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved