logo

NOW ON AIR

Listen in Live

AU: Kiswahili lugha rasmi ya kazi Afrika

Lugha ya Kiswahili imerasmishwa kuwa lugha rasmi katika sehemu za kikazi barani Afrika.

image
na Radio Jambo

Habari14 February 2022 - 07:18

Muhtasari


• Ni rasmi sasa kwamba lugha ya Kiswahili imehalalishwa kuwa lugha rasmi katika sehemu za kikazi barani Afrika.

• Tangazo la kurasmisha lugha ya kiswahili lilitolewa katika bunge la wakuu wa mataifa ya bara Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Vitabu vilivyoandikwa na Gurnah vikiwa katika maonesho

Ni rasmi sasa kwamba lugha ya Kiswahili imehalalishwa kuwa lugha rasmi kakita sehemu za kikazi barani Afrika.

Hii inafuatia ombi lililowasilishwa katika muungano wa mataifa ya Afrika, AU  na naibu rais wa jamhuri ya Tanzania, Philip Mpango kutaka lugha hiyo itambulike rasmi katika sehemu za kazi.

Katika kutetea ombi hilo, Mpango alisema kwamba lugha ya Kiswahili ina watumiaji zaidi ya milioni 100 wanaoifanya lugha hiyo kuwa miongoni mwa lugha zenye wazungumzaji wengi zaidi barani Afrika.

Mpango alikitetea Kiswahili kwa kusema kwamba lugha hiyo imesambaa katika jamii nyingi katika muungano wa Afrika mashariki EAC, muungano na kimaendeleo wa mataifa ya kusini SADC, na vile vile ni lugha ambayo inafunzwa katika mataifa mengi ndani na nje ya Afrika.

Tangazo la kurasmisha lugha ya kiswahili lilitolewa katika bunge la wakuu wa mataifa ya bara Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Itakumbukwa hii si mara ya kwanza kwa wajumbe wengi wa muungano wa AU kusukuma kurasmishwa kwa lugha ya kiswahili na ambapo shirika la UNESCO lilitangaza Julai 7 ya kila mwaka kuwa siku kuu ya Kiswahili duniani.

Kulingana na utafiti wa UN, lugha hiyo ina mizizi yake Afrika Mashariki na uzungumzaji wake umesambaa kwa takribani mataifa 14 yakiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sudan Kusini, Somalia, Mozambique, Malawi, Zambia, Comoros, na mpaka Oman na Yemen katika mashariki ya kati.

Lugha hii ya kiswahili imezidi kukita mizizi huku mataifa kutoka kusini mwa Afrika kama vile Botswana na Jamhuri ya Afrika Kusini wakiwa wameyajumuisha katika mtaala wa masomo huku taifa la Namibia likitarajiwa kujiunga nao.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved