1. Crime and Justice – Series
Kama hujatazama filamu ya Crime and Justice season 1, basi lazima utakuwa unaishi gizani. Mfululizo huu wa filamu ni wa kwanza kabisa kwenye Showmax kuwahi kufanyika nchini Kenya na kichwa chake kilikuwa kati ya vichwa kumi bora vilivyotazamwa kwa jumla zaidi kwenye Showmax nchini Kenya katika mwaka wa 2021. Season 2 ya Crime and Justice inakukujia moto kabisa tarehe 21, Februari mwaka huu 2022.
2. Single Kiasi - Series
Single Kiasi inafuatilia marafiki watatu wasichana jijini Nairobi jinsi wanavyopambana kujipenyeza katika heka heka za maisha jijini. Inajumuisha waigizaji Wakenya Gathoni Mutua anayeigiza kama Sintamei, Minne Kariuki akiigiza kama Mariah na Faith Kibathi akiigiza kwa jina la Rebecca. Tamthilia hii pia inaangazia uhusiano dhabiti wa kirafiki ambao unawashirikisha wanawake hawa, ikijulikana kwamba hata wakati mambo yanawageukia magumu bado watazidi kuwa na ushirikiano huo huo.
3. Baba Twins - Movie
Hii ni tamthilia ya vichekesho inayofuatilia Tony na Wamz, wapenzi wachanga ambao wanajipata katikati ya wimbi la malezi ya wanao mapacha, pindi tu taaluma zao zinaanza kung’oa nanga. Filamu hii ni ya kwanza kabisa kutoka Kenya kuoneshwa kwenye Showmax. Inaongozwa na Lawrence Murage na uzalishaji umefanywa na Lucy Mwangi ambaye pia amezalisha vipindi pendwa vya kuchekesha kwenye runinga kama vile Auntie Boss, Njoro wa Uba na Varshita.
Unaweza ukatazama vipindi hivi na vingine vingi kwenye simu yako ya mkononi au kwa kipakatalishi chako kwenye Showmax kwa bei iliyopunguzwa wakishirikiana na Safaricom. Nunua kwa mwezi wa kwanza na upate mwezi wa pili free #DoubleTheWatch
Kwa mpango bora wa thamani
- Lipa Ksh389 kwa mwezi na upate kutazama Showmax kwa simu moja ya mkononi kwa miezi miwili na unaongezwa data za 1GB
- Kwa 1GB ya data, unaweza ukatiririsha mpaka masaa kumi za sinema za humu nchini, vipindi vya Watoto na vipindi vya kimataifa.
Pia unaweza jipakulia vipindi hivyo na kuvitizama kwa simu au kipatalishi chako wakati uko nje ya mtandao.
Kwa mpango wa thamani ya malipo