Mwanamuziki na muigizaji wa kike Nandy almaarufu The African Princess amepongeza mashabiki wake kwa kufanikisha hafla ya kulipiwa mahari na mumewe Billnass.
Mwanamuziki huyo alilipiwa mahari na Billnas siku ya Jumapili ambapo ilikuwa ni sherehe kubwa nyumbani kwa akina Nandy.
Siku ya Jumatatu, wawili hao walichapisha kanda ya video ambayo ilikuwa inaonyesha Bilnass akipiga magoti chini na kumvisha pete ya uchumba mwamuziki huyo ambapo inaarifiwa kuwa Billnas alitumia milioni 18 za Kitanzania kulipa mahari.
Kupitia ukurusa wa instagram Nandy amepongeza wote waliofanikisha siku hiyo na kuwa ya kuvutia.
“ Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wale wote walio kuwa na sisi siku yetu ya mahari jana neno ASANTE ndilo tunaweza kusema! Vyombo vya habari vilivyotangaza haabari hizo ndani na nje ya nchi hatuna cha kulipa kwa msaada wenu,”Alisema Nandy.
Vilevile aliomba msamaha kwa mashabiki ambao walikuwa na matamanio ya kufika kwenye sherehe hizo lakini hawakuweza kwa sababu ambazo hakuziweka wazi.
“Pia tunaomba radhi kwa wale ambao walitamani kuwa nasi pamoja Jana na haikuwezekana kwa Sababu ziliko nje ya uwezo wetu na wao nyinyi nyote mna umuhimu kwetu siku special na kubwa inafika tutajumuika wote. MUNGU ni Mwema sana na imefanyika kuwa kweli!”