logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilikuwa nacheza densi za roadshow kwa zawadi kama kofia - David Moya

Moya alisema alianza densi katika roadshows na kwanza matukio yote hayaratibiwi.

image
na Radio Jambo

Habari23 February 2022 - 07:34

Muhtasari


• Moya alisema kwamba alikulia Maisha yake Maai Mahiu na alikuwa anaenda kwenye maonyesho ya kando ya barabara maarufu roadshows ili kucheza kwa zawadi ndogo ndogo kama kofia.

• Pia alisema kwamba video zake za TikTok, matukio yote hayapangwi kama baadhi wanavyodai na kwamba wanafanya tu bila kujua matokeo yake yatakuwa yapi.

Mcheza densi maarufu wa TikTok nchini Kenya David Moya amezungumza jinsi safari yake ya kucheza densi za kuburudisha ilianza.

Akizungumza na Mwende na Clemmo Februari 22 kwenye radio, Moya alisema kwamba alikulia Maisha yake Maai Mahiu na alikuwa anaenda kwenye maonyesho ya kando ya barabara maarufu roadshows ili kucheza kwa zawadi ndogo ndogo kama kofia na shati tao zilizopeanwa kwa watazamaji pale.

“Nilikuwa naenda kucheza densi kwa roadshows ambapo walikuwa wanapeana zawadi za kofia kwa watu na nilikuwa wa kwanza kufika huko,” alisema Moya.

Mcheza densi huyo aliingia kwenye mtandao wa TikTok mwaka 2019 ambapo alianza kusambaza video fupi akicheza densi ambapo kufikia sasa amechyukuliwa na wasanii mbalimbali katika video za miziki yao.

“Nimepewa kazi nyingi za kucheza densi katika tasnia ya humu nchini ambapo nimeonekana kwenye video za wasanii kama vile Nameless, Khaligraph Jones na wengine wengi. Pia nime perform kwenye majukwaa ya kitaifa na kimataifa,” alisema Moya.

Moya amekuwa akivizia mtu kwenye mitaa ya Nairobi na kuanza kucheza densi mbele yake bila huyo mtu kutarajia na alipoulizwa kama sarakasi zake hizo za kuvizia zimewahi mpeleka pabaya, alisimulia kisa ambacho kilizua zogo na Maasai mpaka ikabidi wamtulize kwa kununu moja kati ya bidhaa zake.

“Ilikuwa mwanzo mwanzo huko wakati tulikuwa tunafanya skits za karate na tulienda Amboseli ambapo tulijaribu skits hizo kwa wafanyibiashara wamaasai tukajipata pabaya. Lengo letu lilikuwa ni kuburudisha tu lakini wale jamaa hawakuelewa mzaha huo. Nilichukua baadhi ya bidhaa za mfanyibiashara mmoja Maasai na nikarusha chini, wenzake walishirikiana na kutuapiza, mpaka ikabidi tununue rungu yao,” alieleza Moya.

Mcheshi huyo wa TikTok alieleza kwamba video zake zote hakuna yeye hupangiwa na hivo hawajui matokeo yake yatakuwaje ila ni kujaribu tun a baadae inatokea vizuri na watu wanaipenda.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved