logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rayvanny amuonya mwanahabari anayefuatilia Baby mama wake

mwanahabari huyo  amekuwa akieneza habari potovu kuhusu Fahyvanny.

image
na

Burudani25 February 2022 - 04:14

Muhtasari


• Rayvanny  amesajiliwa na Lebo ya Wasafi kwa muda mrefu na kwa mara ya kwanza amezungumzia uhusiano wake na mama wa mtoto wake.

• Amerejea nchini Tanzania baada ya kuwa nje ya nchi kwa zaidi ya wiki mbili ambapo alikuwa ziarani nchini Dubai kutumbuiza mashabiki wake.

 

Mwanamuziki mashuhuri wa bongo fleva,Ravyanny amemuonya mwahabari wa  kituo cha habari cha Wasafi kuacha kufuatilia maisha ya mama wa mtoto wake, Fahyvanny.

Rayvannyy amerejea nchini Tanzania baada ya kuwa nje ya nchi kwa zaidi ya wiki mbili ambapo alikuwa ziarani nchini Dubai kutumbuiza mashabiki wake.

Kupitia ukurusa wake Instastori amesema mwanahabari huyo  amekuwa akieneza habari potovu kuhusu Fahyvanny na kumuomba akome kushughulika na mambo yasiyomhusu.

"Juma Lokole, tafadhali usipite mipaka, usivuke mipaka nakuheshimu sana," alisema Rayvanny.

Vivile aliongeza kuwa anapenda kuweka mambo yake nje ya mtandao na hivyo  hataki jinsi mwanahabari huyo anazungumzia mahusiano yake hadharani kuwalinganisha vidosho wake wake wawili Paula Kajala  na Fahyvanny.

 Ninawapea  heshima wote, hii sio vita wala sio mambo ya mechi za mpira, sipendi na sitawai kuja kupenda."

Rayvanny  amesajiliwa na Lebo ya Wasafi kwa muda mrefu kwa mara ya kwanza amezungumzia mahusiano baina  yake na mama wa mtoto wake, hata hivyo siku jana alithihirisha kwamba wangali na uhusiano na  Fahyvanny.   

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved