logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Dadake Diamond, Queen Darleen amchana mke mwenzake kufuatia migogoro ya ndoa yao

Darleen alisema kuwa kunazo sababu ambazo hushinikiza mwanaume kutafuta mke mwingine.

image
na Radio Jambo

Habari02 March 2022 - 09:30

Muhtasari


•Queen Darleen alisema kuwa kunazo sababu ambazo hushinikiza mwanaume kutafuta mke mwingine.

•Darleen na mke wa kwanza wa mumewe wanafahamika kutokuwa na uhusiano mzuri na siku za hapo awali wawili hao wametupiana vijembe kochokocho.

Queen Darleen na kakake Diamond Platnumz

Mwanamuziki Mwanahawa Abdul Juma almaarufu Queen Darleen ametoa kauli yake kuhusiana na ndoa za wake wengi.

Akiwa kwenye mahojiano na Wasafi Media, Darleen aliweka wazi kuwa hana tatizo lolote na kuolewa katika boma lenye wake wengi.

Katika ujumbe ambao ulisikika kuelekezwa kwa mke wa kwanza wa mumewe Isihaka Mtoro, Queen Darleen alisema kuwa kunazo sababu ambazo hushinikiza mwanaume kutafuta mke mwingine.

"Waislamu tunaruhusiwa kuolewa wanawake hadi wanne. Ndio kaletwa wa pili wewe unaumia, je wengine wakija utafanyaje. Binadamu tunafaa tujue wenzetu wanaletwa kwa sababu gani. Kwa sasa hali ngumu, sio kila mwanaume ambaye anaongeza mke wa pili anafurahia raha, hapana. Kuna vitu ndani yake ambacho tunatakiwa kujua. Mwenyezi Mungu akishaandika eti Queen Darleen atakuwa mke wa pili ndio hiyo ata afanyeje," Alisema.

Kulingana na Darleen, mke wa kwanza hapaswi kulalamikia hatua ya mumewe kuoa mke wa pili ila anafaa kujichunguza kwa undani kilichomsukuma hadi kuchukua hatua hiyo.

Amesema kuwa mke wa kwanza anapaswa kumkubali mke wa pili katika familia ilhali naye wa pili anafaa kumheshimu mwenzake wa kwanza.

"Mke wa pili akiingia, mke wa kwanza anafaa akae chini afikirie imekuwaje mpaka mume wake akaenda kuoa mtu mwingine. Kulalamika haisaidii.  Wewe ukipanic mi akija kwangu namliwaza. Ndio kawaida itakavyokuja mwanaume hataona ghasia kwake hatachelewa kuja, atakaa kwangu kwa sababu anapata malezi na mwendo... unatakiwa uikubali, uibebe na ujue jinsi ya kuendelea mbele. Muache mwenzio aliyeingia aendelee. Haipendezi kuleta unafiki na fitina," Alisema Darleen.

Mwanamuziki huyo hata hivyo alisema kuwa hana uhakika kuhusu hali ya ndoa yake huku akidai kuwa mumewe ndiye aliye katika nafasi nzuri ya kueleza kama bado wako pamoja au la.

Darleen na mke wa kwanza wa mumewe wanafahamika kutokuwa na uhusiano mzuri na siku za hapo awali wawili hao wametupiana vijembe kochokocho.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved