logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nyota wa Nigeria wa Afrobeats Davido: Vitu vingine vinavyonisisimua zaidi ya muziki

Lakini ilipozungumziwa mada ya siasa au shuguli za misaada aliruka na kusimama nje ya kiti.

image
na Radio Jambo

Habari05 March 2022 - 14:15

Muhtasari


  • Lakini ilipozungumziwa mada ya siasa au shuguli za misaada aliruka na kusimama nje ya kiti
  • Muongo mmoja baadaye, Davido yuko London kwa ajili ya tamasha la - O2 arena
davido

Wakati nyota wa Nigeria wa muziki wa Afrobeats star Davido alipokuwa anazungumzia muziki alikuwa mwenye utulivu na asiye na papara.

Lakini ilipozungumziwa mada ya siasa au shuguli za misaada aliruka na kusimama nje ya kiti.

"Nimekuw anikifanya muziki kwa miaka 11," alimwambia DJ wa BBC Edu. "vitu vingine huwa ni ni kama vinananichangamsha zaidi ," aliendelea, huku akisisitiza kuwa bado amejitolea kutengeneza muziki.

Anataka kuingia katika kazi ya kutengeneza Makala na Netflix, ambayo anaielezea kama "ya aina yake".

Davido, ambaye jina lake halisi ni David Adeleke,pia anatengeneza onyesho la mchezo wa Televisheni . '' Ninafurahisha kunitazama," alitania.

Itakuwa "kama Fear Factor" lakini itakuwa na wasichana na kazi. Mshindi anapata "pesa nyingi" na ataweza kwenda kwenye onyesho na yeye.

'Siasa hunipania maumivu ya kichwa'

Nje ya muziki anapenda Habari na siasa, anasema, lakini binafsi hajioni binafsi akibadili kazi yake hivi karibuni kwasababu anasema kila kitu nchini mwake ni fujo.

Nigeriakwa sasa inakabiliwa na upungufu wa mafuta, migomo ya vyuo vikuu, kutoridhika kwa kiasi kikubwa kwa rai ana usalama mbovu katika maeneo mengi yan chi.

"Inanipatia tu maumivu ya kichwa," alisema. "Siwezi kuharibu miaka yangu yote ya burudani, kuwafurahisha watu, halafu nibadilike kuwa mwanasiasa na ndoto zangu zote kama Davido na kila kitu kizuri nilichokifanya kwa ajili yangu kipotee kwasababu hicho ndicho kitakachotokea kiukweli ," alisema.

"Wengi wao waliishia kuharibu jinsi ambavyo wangekumbukwa," aliongeza, akielezea kuhusu watu maarufu ambao waliingia siasa.

Jinsi utakavyokumbukwa ni muhimu kwangu. Anataka kukumbukwa kwa kuwa mtu aliyetengeneza njia, kutoa fursa, kubadili mawazo na Maisha ya watu.

Mwezi Novemba Davido alitoa Naora milioni 250 ($608,000; £450,000) kwa vituo vya mayatima nchini Nigeria baada ya kutuma ujumbe wa Twitter kwa mashabiki wake akiwaomba wampatie pesa iwapo wanaamini kuwa alitoa wimbo uliovuma.

Aliishia kupata pesa zaidi kuliko alizotarajia, ambapo awali aliandika ujumbe wa Twitter uliokuwa zaidi kama mzaha kuliko ombi lenye umakini kla kuomba msaada mashabiki wake wamtumie pesa.

"Nililewa na nikatuma ujumbe wa Twitter wan amba yangu ya akaunti," alisema. Lakini wale walio karibu naye walimshawishi pesa hizo azichukue ziwe zake. "Usiku mzima nilikuwa na watu waliokuwa wananiambia : 'Yo,ni pesa yako'".

Lakini alikuw ani baba yake, bilionea mfanyabiashara Adedeji Adeleke, ambaye alimshawishi Davido kuongeza pesa zake mwenyewe, na kutoa kama msaada.

Ilimchukua miezi mitatu kwake yeye na timu yake kuandaa orodha ya vituo 300 vya yatima ambavyo vilipewa msaada. Anapanga kutoa msaada kila mwaka, alisema.

Mwana wa kiume asiye wa kawaida

Alipoanza katika sekta ya muziki zaidi muongo mmoja uliopita, Davido alisema alichukua njia isiyo ya kawaida akilinganishwa na wengine katika familia yake.

Kwa Adelekes "dhana iliyokuwepo" ilikuwa ni kwenda shuleni na halafu "aende amfanie kazi baba ". Lakini hakufuata mtindo huu.

"Kufariki kwa mama yang una baba yangu kuwa na kazi nyingi kazini ilinipatia muda wa kujitambua binafsi " ana kwamba hapo ndipo muziki ukawa lengo lake. Hata "alishindwa kuendelea " na shule kwasababu ilikuwa inamsumbua.

Lengo lake mapema katika kazi yake lilikuwa ni kufanikiwa sana nchini Marekani kama Akon, lakini baadaye aligundua kuwa sauti ya Kiafrika ndio kilikuwa kitu alichokipenda.

Awali alikuwa mwenye mashaka kuhusu kazi ya muziki ya kijana wake, hakuiamini hadi Davido alipotoa wimbo uliopendwa zaidi wa - Dami Duro mwaka 2012, hapo ndipo baba yake aliona ni umbali gani anaweza kufika kijana wake katika sekta ya muziki.

Kuanzia wakati ule, marafiki wa baba yake ''mabilionea'' walikuwa wakimuita na kumshawishi Bw Adeleke amuache Davido aendelee na muziki. Walipenda sauti yake.

Muongo mmoja baadaye, Davido yuko London kwa ajili ya tamasha la - O2 arena.

Lakini mwanzoni mwa kazi yake, hakuwahi kila mara kuhisi akikaribishwa nchini Uingereza : "Bora ningeenda nyumbani ambako ningetendewa kama mfalme kuliko kwenda kwingine ambako nisingeheshimiwa ."

Lakini , "nyakati ni tofauti", alisema, na muziki wa Afrobeats kwa sasa unapewa heshima unayopaswa kupewa, huku Davido akiwa miongoni mwa nyota kadhaa waliojenga ufuasi wa dunia.

"Huku utamaduni ukiendelea kukua njia zinapanuka, nyimbo zinaendela kutambuliwa,na inafurahisha kuona. Inakuwa ni aina yake ya kipekee ya muiziki, jambo ambalo linafurahisha.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved