logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilikosa kazi nikaamua kuwa mwanablogu - Vinnie Baite

Mcheshi Vinnie Baite amesema kukosa kazi kulimfanya awe mwanablogu.

image
na Radio Jambo

Habari24 March 2022 - 09:31

Muhtasari


• Mcheshi na mwanablogu, Vinnie Baite ameweka wazi sababu yake ya kuamua kuzamia kazi za  mitandao badala kuajiriwa.

• "...Nilijua kupata kazi sio rahisi, kwa hiyo nikaamua kujiajiri mwenyewe," Baite alisema.

Instagram, KWA HISANI

Mcheshi na mwanablogu, Vinnie Baite ameweka wazi sababu yake ya kuamua kuzamia kazi za  mitandao badala kuajiriwa.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha Clouds fm huko Tanzania, Baite alisema kwamba alikosa kazi baada ya kumaliza masomo yake ya chuo kikuu, hivyo kulazimika  kutafuta mbinu mbadala ya kupata hela.

Baite alishikilia kwamba ucheshi na uanablogu unapaswa kuchukuliwa kama kazi zingine rasmi kwa kuwa zimefanikiwa kutoa nafasi za ajira kwa vijana wengi.

"...Nilijua kupata kazi sio rahisi, kwa hiyo nikaamua kujiajiri mwenyewe," Baite alisema.

Kulingana naye, hajuti kabisa kuwa mwanablogu kwa sababu kazi hiyo imempa maisha ambayo angetamani kuwa nayo, na anazidi kupaa katika viwango vya juu.

Aliongezea kwamba kwa sasa ana lengo la kukuza mitandao yake ya kijamii na kupata wafuasi wengi ili kuongeza ushawishi wake wa kibiashara.

Mcheshi huyo pia hakukosa kuwashukuru wale wote ambao wamempa sapoti  tangu anaanza mpaka alipofikia.

Aliwaahidi mashabiki wake kwamba atazidi kutoa kazi nzuri na za kuburudisha.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved