logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Mama alikufa ndani ya nyumba, nilidhani maisha yangu yameisha,' Bahati afunguka jinsi alivyompoteza mamake

Alisema hatua ya kumpoteza mamake ilikuwa pigo kubwa kwake na ilimbadilishia maisha sana.

image
na Radio Jambo

Habari26 March 2022 - 06:53

Muhtasari


•Mwanamuziki huyo amefichua kwamba mamake alifariki siku ya Krismasi ndani ya nyumba  akisubiri zamu yake ya kuhudumiwa hospitalini.

•Bahati alisema hatua ya kumpoteza mamake ilikuwa pigo kubwa kwake na ilimbadilishia maisha sana.

Mwanamuziki Kelvin Kioko almaarufu Bahati amesema analenga kuwakilisha eneo bunge la Mathare ili aweze kuboresha huduma muhimu za jamii katika eneo hilo zikiwemo afya na elimu.

Mzaliwa huyo wa Mathare amesema kuwajengea wakazi wa eneo hilo  hospitali ni jambo la kipaumbele kwake haswa kwa kuwa alimpoteza  mamake kwa kukosa huduma hiyo muhimu.

Mwanamuziki huyo amefichua kwamba mamake alifariki siku ya Krismasi ndani ya nyumba  akisubiri zamu yake ya kuhudumiwa hospitalini. Wakati huo Bahati alikuwa na umri wa miaka sita.

"Kulikuwa na hospitali moja tu ndogo katika eneo la Mathare. Wiki ambayo mamangu alifariki, hata mimi niliwahi kuamka na mtu saa tisa usiku ili tukampangie foleni hospitalini. Hivyo ndivyo mamangu alivyofariki. Mama yangu alikufa wakati mtu mwingine akiwa  amempigia foleni hospitalini," Bahati alisimulia akiwa kwenye mazungumzo na mkewe Diana Marua.

"Alifariki mida ya adhuhuri. Akakaa kwa nyumba kwa masaa kadhaa. Alasiri ilipofika mwili wake ulikuwa umefungwa kwenye blanketi, tukakodishwa teksi ili tumpeleke mochari" Aliendelea.

Bahati alieleza kuwa hatua ya kumpoteza mamake ilikuwa pigo kubwa kwake na ilimbadilishia maisha sana.

"Nilidhani maisha yangu Nairobi yameisha. Nilijua baada ya maziishi ningepelekwa kuishi Ukambani. Huo ndio ulikuwa mpango. Tulikuwa maskini. Baba yangu hangeweza kumudu sisi kuwa na kijakazI... Nilidhani maisha yangu yameisha. Baada ya mazishi nililia sana ili nisiachwe. Nilijificha kwenye gari iliyokuwa imebeba mwili.Nilianza kuishi na jirani," Bahati alisema.

Baadae, mwanamuziki huyo alienda kuishi kwenye Children's Home hadi alipotimiza umri wa kujisimamia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved