logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Kubali kunirudia tafadhali," Harmonize amlilia Kajala hadharani

Frida take me back, I am sorry,” aliandika harmonize kwenye istastories yake

image
na Radio Jambo

Habari29 March 2022 - 06:49

Muhtasari


• Frida take me back, I am sorry,” aliandika harmonize kwenye istastories yake

Mkurugenzi mkuu wa Konde Gang, Harmonize

Harmonize, mkurugenzi mkuu wa rekodi lebo ya Konde Gang mwisho wa siku amefungua roho na kuweka wazi kwamba anamkosa sana muigizaji Frida Kajala katika maisha yake kama mpenzi.

Harmonize katika siku za hivi karibuni amekuwa akiachia jumbe tata zisizoeleweka kuhusu mapenzi na kila mtu anashuku huenda huba lake na mwanadada mzungu Briana huenda haliko sawa kabisa.

Msanii huyo katika jumbe ambazo amekuwa akiachia, zinaonesha kabisa kwamba anaishi maisha ya upweke na ambapo anamtaka sana kurudiana na Kajala kuliko mpenzi mwingine yoyete kati ya wale ambao amekuwa nao.

Baada ya maneno kuzagaa kutokana na bango kubwa lililoonekana na picha ya pamoja ya Harmonize na Kajala likifuatishwa na neno ‘Lovers’ wengi walishindwa kuelewa maana hasa ya bango hilo lakini hatimaye Harmonize ametema nyongo na kusema kwamba anataka kurudiana na mwanamama Frida Kajala.

“Frida take me back, I am sorry,” aliandika harmonize kwenye istastories yake na kisha baadae kuufuta ujumbe huu.

Kwa kuachia ujumbe kama huu wa moja kwa moja bila kuficha, inaonesha ni kwa kiasi gani msanii huyo amesongwa na upweke mpaka kufikishwa mwisho wa kona ambapo amelazimika kufichua bila kujali jamii itamchukuliaje, mwanzo Kajal amemuacha sana kiumri, na pili walikosana kwa kile kilichosemekana ni msanii huyo kutaka kuvizia kuku na kifaranga wake, kwa maana ya Kajala na bintiye Paula.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved