logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Nilishinda bet ya SportPesa nikalipa mahari na kujenga choo" - Zablon Shitanda

Zablon - Kwa hiyo pesa niliweza kupeana mahari ya ng’ombe, hata sasa hivi nimejenga bafu na choo.

image
na Radio Jambo

Burudani30 March 2022 - 10:06

Muhtasari


• Nilishinda shilingi elfu 238 kutoka jukwaa la SportPesa. Kwa hiyo pesa niliweza kupeana mahari ya ng’ombe, hata sasa hivi kwa boma yangu nimejenga bafu na choo ya SportPesa

Zablon Shitanda, mshindi wa jackpot ya SportPesa

Mwanaume mmoja kutoka kaunti ya Kakamega amewafurahisha watumiaji wa mtandao wa Twitter wakati alipoweka wazi kwamba baada ya kushinda mchezo wa kamari katika jukwaa la SportPesa, aliamua kutumia kiasi hicho kulipa mahari ya mkewe na masalio kujenga bafu na choo.

Zablon Shitanda, mwenyeji wa Malaba aliwekeza katika mchezo huo wa spoti na kujishindia kiasi cha elfu 238,778 pesa za Kenya mnamo mwezi wa tisa mwaka jana na kusema kwamba hajutumii kwa jinsi alivyoratibu matumizi ya hela hizo.

“Mimi ni shabiki wa SportPesa niliweza kuwekeza na juzi mwezi wa tisa nilishinda shilingi elfu 238 kutoka jukwaa la SportPesa. Kwa hiyo pesa niliweza kupeana mahari ya ng’ombe, hata sasa hivi kwa boma yangu nimejenga bafu na choo ya SportPesa,” anasikika akisema katika video ambayo jukwaa hilo kubwa la ubashiri nchini lilipakia kwenye ukurasa wao wa Twitter.

Katika video hiyo, watu wametoa maoni yao tofauti tofauti. Kuna wale wanaompongeza kwa hatua hiyo ya kutumia pesa kwa mambo ambayo yanaweza elezeka kwa miaka na mikaka ijayo huku baadhi wakitofautiana na yeye kwa kusema kwamba angenunua kwanza simu nzuri.

Ama kwa kweli watu hawafanani katika fikira na mawazo!

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved