logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Polisi wanne watiwa mbaroni kwa madai ya ufisadi

kujifanya maafisa kutoka Mamlaka ya Kukusanya Ushuru (KRA) na NEMA kisha kutumia fursa hiyo kutekeleza uhalifu wa ufisadi katika mtaa wa Ongata Rongai.

image
na Radio Jambo

Habari09 April 2022 - 06:34

Muhtasari


•Walijifanya maafisa kutoka Mamlaka ya Kukusanya Ushuru (KRA) na NEMA kisha kutumia fursa hiyo kutekeleza uhalifu wa ufisadi katika mtaa wa Ongata Rongai.

Maafisa wanne kutoka kituo cha polisi cha Kamukunji wapo kizuizini baada ya kukamatwa kwa madai ya ufisadi.

Oburo, Dorcas Nzilani na Winfred Kanana wanaripotiwa kutelekeza majukumu yao na kujifanya maafisa kutoka Mamlaka ya Kukusanya Ushuru (KRA) na NEMA kisha kutumia fursa hiyo kutekeleza uhalifu wa ufisadi katika mtaa wa Ongata Rongai.

Kitengo cha DCI kimeripoti kwamba, washukiwa, bila idhini yoyote waliondoka kituoni na kuenda kukamata wafanyibiashara wawili kwa madai ya kuwa na karatasi za plastiki.

Maafisa hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi huku uchunguzi zaidi ukiendelea kabla yao kuadhibiwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved