logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hana namna! Babalevo asema Kajala atamrudia Harmonize

Babalevo amesema kwamba Kajala atamsamehe Harmonize na wafufue penzi lao.

image
na Radio Jambo

Habari11 April 2022 - 05:51

Muhtasari


• Babalevo amesema kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa Harmonize kumnasa Kajala.

• Alishikilia kwamba Kajala ana mapenzi mengi kwa Konde.

Msanii na mtangazaji kutoka Tz, Babalevo amesema kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa Harmonize kurejeleana na mpenzi wake wa zamani, Frida Kajala.

Alisema kwamba licha ya mambo mabaya aliyoyapitia Kajala kipindi yupo kwenye mahusiano na Konde, kuna ishara tosha kwamba atamsamehe na kukubali kufufua penzi lao.

"...Unazungumzia Kajala sio? Ninavyoona atakubali kurudiana na Harmonize," Babalevo alisema.

Babalevo alisema kwamba ni rahisi kwa mwanamke kusamehe mwanaume anapofanya kosa, kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa Kajala akakubali kuyeyusha moyo na kuliendeleza penzi lao.

Ikumbukwe Harmonize alikiri kwamba ameshindwa kufunga katika kipindi hiki cha Ramadhan kwa sababu ana mawazo mengi kuhusu Kajala na angependa sana kumnasa tena katika himaya yake ya huba.

Licha ya vurugu zilizotokea wakati wanatengana, ni wazi kwamba penzi kati yao lilikuwa limekolea sana.

Mpaka sasa Kajala hajatoa tamko lolote iwapo angependa kurejeleana na 'tembo' , huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona hatua atakayoichukua.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved