logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mume wa mwimbaji wa Nigeria aliyefariki Osinachi Nwachukwu akamatwa

Haijabainika iwapo Bw. Nwachukwu ametoa maoni yake kuhusu kukamatwa kwake.

image
na Radio Jambo

Habari11 April 2022 - 13:27

Muhtasari


  • Mume wa mwimbaji wa Nigeria aliyefariki Osinachi Nwachukwu akamatwa

Mume wa marehemu mwimbaji wa nyimbo za Injili wa Nigeria Osinachi Nwachukwu amekamatwa kufuatia kifo chake, vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti.

Osinanchi, 42, alipoteza maisha siku ya Ijumaa akiwa hospitalini katika mji mkuu, Abuja.

Ripoti za awali zilisema kuwa mwimbaji huyo maarufu alikuwa akiugua saratani ya koo, lakini familia yake inakanusha hilo, ikidai kuwa alikuwa mwathirika wa unyanyasaji wa nyumbani.

Lakini Msemaji wa polisi mjini humo amenukuliwa na tovuti za Daily Trust and Punch akithibitisha kukamatwa kwa Peter Nwachukwu baada ya malalamiko kutoka kwa kaka yake mwimbaji huyo.

Haijabainika iwapo Bw. Nwachukwu ametoa maoni yake kuhusu kukamatwa kwake.

Osinachi alipata umaarufu 2017 kwa wimbo wa injili Ekwueme aliouimba na Prospa Ochimana.

Pia alikuwa mwimbaji mkuu Dunamis International Gospel Centre.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved