logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Woiye!Wanamitandao wamkejeli aliyekuwa mpenziwe Stivo Simple Boy

Vishy amesema kuwa ana sifa kemkem zinazofanya astahiki kiasi hicho kikubwa cha fedha

image
na Radio Jambo

Habari11 May 2022 - 10:14

Muhtasari


  • Wanamitandao wamkejeli aliyekuwa mpenziwe Stivo Simple Boy

Mpenzi wa zamani wa mwanamuziki Stivo Simple Boy, Purity Vishenwa almaarufu Pritty Vishy ametangaza kuwa mwanaume anayekusudia kumuoa ni sharti awe tayari kulipa mahari ya shilingi milioni mbili.

Akiwa kwenye mahojiano na Nicholas Kioko, Vishy aliweka wazi kuwa hataki mume wake mtarajiwa awape wazazi wake ng'ombe kama mahari yake.

Kipusa huyo amesema mume wake mtarajiwa anapaswa kuwapatia wazazi wake gari badala ya ng'ombe.

"Mahari yangu ni milioni mbili. Na mtu asijaribu kuniletea ng'ombe. Sitaki ng'ombe zinaletwa kwetu. Mimi ni milioni mbili, tosha! Kama unataka kuleta ng'ombe basi hiyo pesa ununue gari. Hiyo pesa ya ng'ombe unafaa kuchanga ununue gari ulete," Vishy alitangaza.

Vishy amesema kuwa ana sifa kemkem zinazofanya astahiki kiasi hicho kikubwa cha fedha kama mahari.

Hata baada ya kujiamini wanamitandao hawakulaza damu bali walimkejeli Vishy kwa matamshi yake ya mahari;

Hizi hapa baadhi ya kejeli hizo;

bedanbido: 😂😂😂nono round😂😂Matycoon wanataka watu wako slimmmm 😂😂💣

steve_.g._official._: Acha nicheke😂😂😂 hi ni confidence ya wapi hii😂

tashamuthonime: naona tu upate wa kulipa hiyo dowry kwanza amount utasema akishapatikana😂

n.o.t.o.r.i.o.u.s_biggie: 😂 two miliion kwani usiku unageuka nikki minaj😂🚮


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved