logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Bosi wangu ndiye G.O.A.T" Mtangazaji Diva ammiminia Diamond Platnumz sifa kochokocho

Diva amefichua kuwa Diamond ameahidi kumtimizia ndoto yake ya kumiliki gari aina ya BMW.

image
na Radio Jambo

Habari18 May 2022 - 07:07

Muhtasari


•Diva amefichua kuwa bosi wake Diamond Platinumz amekuwa akimthamini sana tangu alipojiunga na Wasafi takriban mwaka mmoja uliopita.

•Amesema anawapenda sana wafanyi kazi wenzake katika Wasafi Media wamekuwa nguzo muhimu katika maisha yake.

Diva The Bawse na Diamond Platnumz

Mtangazaji maarufu nchini Tanzania Diva The Bawse ameweka wazi kuwa anafurahia sana kufanya kazi katika Wasafi Media.

Akiwa kwenye mahojiano na waandishi wa habari, Diva alifichua kuwa bosi wake Diamond Platinumz amekuwa akimthamini sana tangu alipojiunga na Wasafi takriban mwaka mmoja uliopita.

"Sio tu suala la mshahara. Nilipoingia pale Diamond alinipatia kila kitu. Kwenye harusi yangu alinipatia mengi sana. Bosi wangu ndiye mkubwa zaidi wakati wote," Diva alisema.

Mtangazaji huyo amefichua kuwa Diamond ameahidi kumtimizia ndoto yake ya kumiliki gari aina ya BMW.

"Niliambia bosi wangu kuwa nahitaji BMW. Alisema atanipatia. Yeye ndiye atanunua. Bosi wangu hatakangi watu wake tupate shida," Alisema.

Diva pia alisema alipokewa vizuri sana alipojiunga na Wasafi na amedai mazingira aliyopata pale yamemleta raha moyoni.

Alisema anawapenda sana wafanyi kazi wenzake katika Wasafi Media wamekuwa nguzo muhimu katika maisha yake.

"Wanasapoti sana. Wakati vitu vingi vimekuwa vikiendelea wamekuwa wakinijulia hali. Kutoka nifike Wasafi nina amani, nina raha, nina furaha. Zamani sikuwa na raha. Kwa sasa nina raha. Nawapenda wafanyikazi wenzangu, kwangu wao ni familia yangu," Diva alisema.

Diva ameweka wazi kuwa wafanyikazi wenzake wamemkubali kabisa na wanaelewa mtindo wake wa maisha.

Aidha Diva amesisitiza kuwa kwa sasa yeye ndiye wa pili kwa umaarufu nchini Tanzania baada ya Diamond.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved