logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(Video) Polisi watambua jamaa aliyeuawa kwa kupigwa risasi Kasarani

Polisi walisema Samuel Mugo Mugota mwenye umri wa miaka 49 alikuwa na historia ya uhalifu.

image
na Radio Jambo

Habari18 May 2022 - 07:41

Muhtasari


• Polisi walisema alikuwa na vitambulisho saba kwenye gari lake alipopigwa risasi na kuuawa Jumatatu mchana na mtu asiyejulikana.

• Alipigwa risasi kwa karibu baada ya kusimamishwa na watu wasiojulikana akiendesha gari aina ya Honda CRV.

• Jamaa aliyempiga risasi alitoroka katika gari lililokuwa limeegeshwa mbele ya gari la marehemu.

Polisi wamemtambua mwanamume aliyepigwa risasi na kuuawa kwenye gari eneo la Mirema, Kasarani kama Samuel Mugo Mugota mwenye umri wa miaka 49 na kwamba alikuwa na historia ya uhalifu.

Polisi walisema alikuwa na vitambulisho saba kwenye gari lake alipopigwa risasi na kuuawa Jumatatu mchana na mtu asiyejulikana.

Mwanamke mmoja ameambia polisi kuwa kitambulisho chake na hati za benki zilizotumiwa kuiba shilingi 360,000 kwenye akaunti yake ya benki zilipatikana ndani ya gari la jamaa huyo.

Polisi walisema alikuwa akifuatiliwa na wapelelezi kwa sababu za kubadilisha nambari za simu kila wakati na sakata ya ulaghai wa pesa 'wash wash'.

Alipigwa risasi kwa karibu baada ya kusimamishwa na watu wasiojulikana akiendesha gari aina ya Honda CRV.

Jamaa aliyempiga risasi alitoroka katika gari lililokuwa limeegeshwa mbele ya gari la marehemu.

Wakati huo huo, Polisi wanachunguza tukio ambapo mwanamume mmoja alidungwa kisu na kujeruhiwa vibaya na wanaume wawili wanaoaminika kuwa wanachama wa kundi la wapenzi wa jinsia moja (LGBTQ) wakiwa katika chumba cha kulala wageni katikati mwa jiji.  

Polisi wanasema wanaume wawili walikodi chumba kwanza kwenye nyumba hiyo kabla ya kuungana na wa tatu. Akiwa humo, yalizuka mapigano baina yao kabla ya wawili kumgeukia mmoja na kumdunga kisu tumboni na kutoroka. 

Mmoja wao hata hivyo alikamatwa baadaye walipokuwa wakijaribu kutoroka na kuwaambia polisi kwamba walikosana wakiwa chumbani na kusababisha makabiliano hayo.  Aliwaambia polisi kuwa ni wanachama wa kundi la wapenzi wa jinsia moja.

Polisi walisema majeruhi alipelekwa hospitalini ambako yuko chini ya uangalizi huku mshukiwa akitarajiwa mahakamani kujibu mashtaka mbalimbali.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved