logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Mimi ni mgonjwa sana!" Wema Sepetu afunguka kuhusu ugonjwa unaomuathiri

Ndugu za Diamond, Esma Platnumz na Rommy Jons ni miongoni mwa watu waliomtakia afueni.

image
na Radio Jambo

Habari30 May 2022 - 17:34

Muhtasari


•Wema Sepetu  amesema anaugua sana huku akifichua kuwa Malaria katika mwili wake iko katika kiwango cha 80.

•Wema alifichua kuwa uchungu mdomoni ni mojawapo ya dalili ambazo anashuhudia kutokana na ugonjwa huo.

Muigizaji na mwanamitindo maarufu kutoka Bongo Wema Sepetu anaendelea kupata afueni baada ya kushambuliwa na maradhi.

Jumatatu mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz alifichua kuwa anaugua ugonjwa wa malaria.

Wema alisema anaugua sana huku akifichua kuwa Malaria katika mwili wake iko katika kiwango cha 80.

"Mimi ni mgonjwa sana... Malaria 80, UTI ya Kutosha, Damu ipo 6.. nitaona pilipili," Wema alisema kupitia Instagram.

Muigizaji huyo aliambatanisha ujumbe wake na video inayoonyesha akiwa anapokea matibabu katika hospitali.

Wema alisikika akilia kwa sauti huku daktari akisukuma sindano kwenye mshipa wa mkono wake wa kulia.

"Sindano zinauma hizi kweli jamani," Alisema Wema.

Mlimbwende huyo alifichua kuwa uchungu mdomoni ni mojawapo ya dalili ambazo anashuhudia kutokana na ugonjwa huo.

Mamia ya wanamitandao wakiwemo watu mashuhuri walimtakia muigizaji huyo afueni ya haraka.

Ndugu za Diamond, Esma Platnumz na Rommy Jons ni miongoni mwa watu waliomtakia afueni muigizaji huyo.

@_esmaplatnumz Pole machungwa unatumia?

@romyjons Na ukatulie kwenye ndoa dadangu

@luismunana Nakutumia hug kubwa

Malaria ni ugonjwa wa kuambukiza ambao unaenezwa na mbu wa jenasi Anopheles na kusababishwa na kidubini aina ya protisti Plasmodium. Ni ugonjwa ambao una tiba lakini unaendelea kusababisha vifo vingi duniani.

Ni muhimu kutembelea kituo cha afya punde baada ya kushuhudia daliili zinazohusiana na ugonjwa huo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved