logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ndoa ni ngumu,hakuna mbaba anataka msichana mzee-Risper Faith asema huku akiwashauri wanawake haya

Ni swali ambalo lina majibu tofauti, na kila mtu ana maono yake kuhusu jambo hilo.

image
na Radio Jambo

Habari17 June 2022 - 10:14

Muhtasari


  • Mwanasosholaiti Risper Faith kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewashauri wanawake hasa wenye wana umri wa miaka 20

Je umewahi jiuliza mbona wanawake wengi wako single hasa karne hii na wanaendelea vyema?

Ni swali ambalo lina majibu tofauti, na kila mtu ana maono yake kuhusu jambo hilo.

Mwanasosholaiti Risper Faith kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewashauri wanawake hasa wenye wana umri wa miaka 20.

Kulingana na mwanasosholaiti huyo wanawake hao wanapaswa kuwachumbia wanaume tofauti kwani watakapohitimu miaka 30, na kutaka kutlia kwenye ndoa hawatasumbuana na weni wao.

Kulingana na Risper hamna mbaba ambaye anatamani msichana mzee, hivyo basi aliwashauri mashabiki wake wanawake wafanye mazoezi wakiwwa na miaka 20 ili wasikae kuzeeka ilhali ni wachanga.

"Chumbiana na wanaume wengi kuwa smart-wekeza katika kitu-kwenda kwenye ukumbi wa mazoezi na ujenge mazoea ili katika miaka yako ya 30 uizoea.-fanya mahusiano yenye maana na marafiki zako -usijifungie ndani ya nyumba toka mara kwa mara-usibebe mimba-oa mwanamume ambaye amefichuliwa na ana mali zake nyingi katika majina yenu yote

Nina mengi ya kushiriki kuhusu hili. Sababu ya kwanini nasema date wavulana wengi ni kwa sababu wakati unataka kutulia utakuwa unajua ni nani anayefaa zaidi ... miaka ya 20 ni umri wako mkuu kwa sababu wavulana wengi wanapendelea wasichana kati ya umri wa miaka 23-28. miaka kwa hivyo furahiya miaka hiyo na ufaidike zaidi nayo. wakati unaadhimisha miaka 30 anza kutulia .akuna mbaba anataka msichana mzee ukweli mchungu."

Mmmoja wa mashabiki wake alimuuliza Risper kama ndoa ni ngumu na jibu lake lilikuwa;

"Ndio ndoa ni ngumu," Alijibu Risper.

Ndoa ni ngumu-Risper Faith asema huku akiwashauri wanawake haya

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved