logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ndoa zitavunjika!DCI yafichua kwa nini hawatoi matukio ya kusisimua yaliyofanyika Naivasha

DCI ilibainisha kuwa Wakenya wengi wangemwaga machozi ikiwa wangetoa ripoti hiyo

image
na Radio Jambo

Habari27 June 2022 - 11:43

Muhtasari


  • DCI yafichua kwa nini hawatoi matukio ya kusisimua yaliyofanyika Naivasha

Baada ya kuahidi kutoa ripoti ya kina kuhusu drama iliyotokea Naivasha wakati wa Safari Rally wikendi, DCI amebatilisha kazi hiyo baada ya mkuu wa DCI George Kinoti kuingilia kati.

Timu ya mawasiliano ya DCI ilikuwa imeahidi kutoa kila undani wa kile kilichotokea Naivasha, lakini kwa minajili ya amani katika ndoa, wameghairi kumwaya mtama huo.

Kwenye mitandao ya kijamii, DCI ilibaini kuwa walikuwa na uzi wa kina wakisimulia jinsi drama  zilivyotokea, lakini kabla ya kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii, bosi wa DIC Kinoti aliingilia kati na kusitisha misheni hiyo.

DCI ilibainisha kuwa Wakenya wengi wangemwaga machozi ikiwa wangetoa ripoti hiyo na kwamba ndoa nyingi zingeweza kuvunjika kabla ya wakati wake.

"Vinginevyo mkuu Kinoti amesema tukanyagie hadithi hiyo ya Vasha. Vile admin hajalala akiunda thread, ingekuwa premium tears. Ndoa zingevunjika. Ama tupatie," Timu ya mawasiliano ya DCI ilibainisha.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved