logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Kuuza bangi kutajenga Expressway 2 katika kila kaunti" - Wajackoyah

"Kuuza bangi kutaleta pato la kujenga Expressway 2 kila kaunti kando na kununua kampuni ya Microsoft chini ya miaka 2 pekee" - Wajackoyah

image
na Radio Jambo

Habari01 July 2022 - 04:57

Muhtasari


• "Kama tutapanda bangi katika kaunti ya Nyeri pekee basi wakaazi wakatengeneza pesa kiasi cha shilingi trilioni 4.6 kwa kila vuno.”

Msomi Wajackoyah ambaye analenga kuchaguliwa kama rais wa tano katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9 amefafanua zaidi na kuitetea manifesto yake ya kupa kipaumbele suala la ukulima wa bangi.

Akilizamia suala hilo zaidi wakati wa uzinduzi wa manifesto yake Alhamisi usiku katika ukumbi wa KICC, Wajackoyah alielezea manufaa ya mmea huyo ambao hadi sasa hivi bado umeharamishwa nchini na kusema kwamab iwapo atachaguliwa basi serikali yake itaupa upanzi wake kipaumbele zaidi ili kulipa madeni ya taifa.

“Ekari moja ya bangi inaweza ikakuzalishia milioni 8 kwa kila vuno, kila vuno huchukua muda wa miezi sita pekee. Kama tutakuwa na mavuno mara mbili kwa mwaka inamaanisha tutapaka milioni 16.” Alisema Wajackoyah.

Msomi huyo akitolea mfano wa kaunti ya Nyeri ambao inasemekana ndio sehemu yenye rotuba nzuri ya kukua kwa mmea huyo, Wajackoyah alisema Kenya inaeza ikapanda bangi katika kaunti hiyo pekee na mazao yake yakauzwa nje ya nchi ya kutumika kama pato la kitaifa pasi na kufanya kitu kingine chochote.

“Kaunti ya Nyeri yote ina upana wa ekari 583,000, hii inamaanisha kwamba kama tutapanda bangi katika kaunti ya Nyeri pekee basi wakaazi wakatengeneza pesa kiasi cha shilingi trilioni 4.6 kwa kila vuno.” Alisema Wajackoyah.

Akitumia lugha ya kibiashara nqa kiuchumi zaidi, wakili msomi alisema kwamba kwa mwaka kaunti ya Nyeri pekee kwa mwaka itazalisha shilingi trilioni 9.2 kutoka kwa mauzo ya bangi nje ya nchi, kiasi ambacho alisema ni sawa na pato la ndani la nchi ya Ethiopia.

Akielezea zaidi na kuitetea manifesto yake ya bangi, profesa Wajackoyah alizama zaidi na kusema kwamba pato hilo hilo kutoka kuuza bangi kutoka kaunti ya Nyeri pekee litakuwa baraka kwa Kenya kwani kila Mkenya atakuwa anapokea mgao wa laki mbili kila mwaka kutoka kwa mauzo ya kuuza bangi kutoka kaunti ya Nyeri pekee yake.

Pia alisema kwamba kutokana na hesabu za takwimu yake, kukuza bangi katika kaunti ya Nyeri pekee yake kutazalisha pesa za kujenga barabara mbili aina ya Expressway katika kila kaunti nchini Kenya na pia kununua kampuni ya Microsoft chini ya miaka miwili pekee.

Maoni yako ni yepi kuhusu ajenda ya bangi ya Wajackoyah?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved