logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Polisi wa trafiki ashindwa kuelezea alivyopata pesa 10.5M, mashamba ya thamani 19.4M, magari

Jaji Mwangi alimtaka inspekta Mulei kuilipa serikali kiasi cha shilingi milioni 10.5, kiasi sawa na pesa zilizopatikana katika benki zake nne

image
na Radio Jambo

Habari14 July 2022 - 10:10

Muhtasari


• Mahakama iliamuru tume ya kuchukua mali za wizi kupiga tanji akaunti zake pamoja na mali nyingine.

• Polisi huyo alipatikana na milioni 10.5 kwenye benki nne, magari matano, mashamba saba na pikipiki ambazo alishindwa kusema alivipataje.

Mchoro wa afisa wa trafiki

Inspekta mmoja mkuu wa kitengo cha trafiki huenda atapoteza mali yake yenye thamani ya mamilioni ya pesa baada ya kushindwa kuielezea mahakama jinsi alivyojizolea utajiri huo mkubwa unaozidi kiasi cha mshahara wake.

Kulingana na chapisho katika gazeti moja la humu nchini, mahakama kuu iliipa tume ya kupambana na wafisadi kupiga tanji akaunti zake zote pamoja na kushikilia mali hiyo hadi pale ukweli wa jinsi alivyoipata utatolewa.

Inspekta huyo kwa jina Gabriel Mbiti Mulei huenda akapoteza kiasi cha milioni 10.5 pesa za benki kuu ya Kenya ambazo ziko katika benki nne tofauti, mashamba manne yanayosemekana kuwa na thamani ya jumla ya shilingi milioni 19.4 pamoja na magari Matano na pikipiki moja.

Katika kesi hiyo iliyopelekwa mahakamani dhidi ya Inspekta Mulei na tume ya kupambana na ufisadi ya EACC mnamo mwaka 2015, jaji Njoki Mwangi alisema mali hizo zote zimeshindwa kubainishwa jinsi gani zilipatikana katika umilisi wa inspekta huyo wa trafiki.

Jaji Mwangi alimtaka inspekta Mulei kuilipa serikali kiasi cha shilingi milioni 10.5 katika siku 30 zijazo, kiasi ambacho ni sawa na pesa zilizopatikana katika benki zake nne. Uchunguzi ulionesha pesa hizo ziliwekwa kweney akaunti hizo kati ya mwaka 2008 na 2011.

Mashamba hayo yanasemekana kuwa katika maeneo ya Kwale na Malindi ambako alihudumu kwa muda kama inspekta wa trafiki.

Afisa huyo aliajribu kuielezea mahakama kwamba utajiri wake ni kutokana na mshahara wake pamoja na pesa alizopokezwa kutoka kwa mashindano ya kulenga risasi ila bado maelezo yake hayakuweza kujenga dhana kwamba kutoka hapo tu angeweza kukuza mtaji wa kiasi hicho.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved