logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kero la Tumbili Likuyani

''Hawa wanyama wameongezeka mno, na wanaruka tu kwa miti wakiona mtu akikuja shambani ''

image
na Radio Jambo

Habari15 July 2022 - 05:45

Muhtasari


•Kwa sasa Wakenya wanakabiliwa na  hali ngumu ya maisha kufuatilia bei ghali za bidhaa hapa nchini.

•Wakulima kutoka pande hiyo walikuwa  wamejawa na hofu kuhusu jinsi watakao lipa madeni za mkopo

Tumbili

Wakulima kutoka Kijiji cha Musutsu kata ya Lumakanda Kaunti ndogo ya Lukiyani wamelalamikia kuhangaishwa na Tumbili ambao wametoroka  kwenye Msitu ya eneo hilo na kuvamia mashamba yao huku wakitekeleza uharibifu mkubwa .

Wakiongoza na Kerani Kihima na Joshua Mbaya wakulima hao walisema kuwa baadhi ya Mimea ambazo zimeharibiwa na Mnyama huyo ni pamoja na Mahindi,,Mboga, Ndizi na Miwa miongoni mwa mimea mengine.

''Hawa wanyama wameongezeka mno, na wanaruka tu kwa miti wakiona mtu akikuja shambani, kazi yao kubwa ni kuharibui Mimea, ''Kerani alisema.

Wakulima hao walisema kuwa huenda hali ya njaa itaongezeka katika eneo hilo kwani tegemeo lao ya kiuchumi panaharibiwa na Tumbili.

Wakulima kutoka pande hiyo walikuwa  wamejawa na hofu kuhusu jinsi watakao lipa madeni za mkopo ambao wengi wao walikopa kutoka kwa Benki tofauti hapa nchini kwa mnajili ya kufanya ukulima.

''Hakuna Mahindi hapa,ona ata hizi zenye zimeanguka chini, Ndizi vile vile  na Mboga ,hapa hatutakuwa na mazao hata kidogo''Joshua alisema.

Wakulima hao sasa wametoa wito kwa Maafisa wa Wanyamapori kuingilia kati na kuwasaidia kuwaondoa Wanyama katika eneo hilo.

Kwa sasa Wakenya wanakabiliwa na  hali ngumu ya maisha kufuatilia bei ghali za bidhaa  msingi  hapa nchini.

Hali ambayo pia imewasukuma kulilia Serikali kuingia kati ilikupunguza bei za bidhaa msingi kama vile Unga, Mafuta, Sukari miongoni mwa bidhaa zingine.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved