logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maafisa wa usalama kurejesha amani ndani ya Molo

Visa vya ukatili vimeshuhudiwa sana maeneo ya Molo

image
na Radio Jambo

Habari22 July 2022 - 09:02

Muhtasari


•Hapo jana wakaazi kutoka vijiji vya Mutirithia na Miti mirefu walipata fursa ya kutangamana na maafisa wa usalama  mjini Molo

•Pia wamewataka viongozi wa maeneo hayo kuhakikisha kuwa  maeneo mengi kumewekwa taa za barabarani na ufyekaji wa vichaka kando ya barabara

Taarifa kuhusu usalama huko Molo zinahofia kuwa kuna uwezekano wa makundi haramu kufurushwa katika operesheni zinazoendelea katika maeneo mengine ya mji wa Nakuru huenda yakahamia Mashinani.

Kulingana na Kamishna Msaidizi wa Kaunti Ndogo ya Molo Steve Ondote kuongezeka kwa ukosefu wa usalama katika vijiji vya Mooto na Mutirithia ni jambo la kutisha na kuwahakikishia wakazi wa eneo hilo usalama wao kwani wamejitolea kurejesha usalama katika eneo hilo.

Haya yanajiri wiki moja baada ya msururu wa mashambulizi dhidi ya wakaazi wa vijiji hivyo viwili na magenge yenye silaha, ambapo vyombo vya usalama huko Molo vimekuwa vikiendesha operesheni za ulinzi wa mashirika mbalimbali usiku.

Hapo jana wakaazi kutoka vijiji vya Mutirithia na Miti mirefu walipata fursa ya kutangamana na maafisa wa usalama  mjini Molo wakitoa hoja zao kutokana na kukithiri kwa ukosefu wa usalama eneo hilo.

Kulingana na wakazi hao walikubaliana kushiriki  na kutoa habari kuhusu kundi hilo la kuhakikisha hatua  mwafaka umechukuliwa ya kuhakikisha kesi hizo hazizidi kuongezeka.

Pia wamewataka viongozi wa maeneo hayo kuhakikisha kuwa  maeneo mengi kumewekwa taa za barabarani na ufyekaji wa vichaka kando ya barabara ambazo zimebainishwa kuwa chanzo cha kukithiri kwa ukosefu wa usalama.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved