logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Neymar akabiliwa na kesi ya ulaghai Barcelona

Kesi hiyo itafanyika mwezi mmoja kabla ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

image
na Radio Jambo

Habari28 July 2022 - 04:28

Muhtasari


•Neymar ​​anakabiliwa na kesi ya madai ya ukiukwaji wa taratibu za uhamisho kutoka Brazil kwenda Barcelona.

•Marais wawili wa zamani wa Barcelona, ​​Josep Maria Bartomeu na Sandro Rosell, pamoja na wazazi wa Neymar wanakabiliwa na madai sawa,

Miaka tisa baada ya mwanasoka Neymar kuhama kutoka Brazil kwenda Barcelona,​​anakabiliwa na kesi ya madai ya ukiukwaji wa taratibu za uhamisho huo.

Katika sakata ya kisheria ambayo imedumu kwa miaka mingi, mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye sasa anachezea Paris Saint-Germain anatuhumiwa kwa udanganyifu na ufisadi.

Kesi hiyo itafanyika kwa wiki mbili kuanzia tarehe 17 Oktoba, mwezi mmoja kabla ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

Watu wengine kadhaa pia watashtakiwa .

Marais wawili wa zamani wa klabu ya soka ya Barcelona, ​​Josep Maria Bartomeu na Sandro Rosell, pamoja na wazazi wa Neymar wanakabiliwa na madai sawa, kulingana na ripoti za Uhispania.

Wale wote waliohusika katika kesi hiyo kwa muda mrefu wamekanusha madai hayo, yaliyotolewa na mfuko wa uwekezaji wa DIS, ambao ulidai kuwa ulikuwa na haki ya kupata 40% ya ada ya uhamisho ya Neymar 2013 alipoondoka klabu ya Santos ya Brazil.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved