logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mkewe Chameleone atoa ushahidi wa kutisha kuthibitisha shemejiye Weasel amekuwa akimdhulumu mkewe

Bi Sandra alionekana kuwa na michibuko kwenye sehemu mbalimbali za mwili.

image
na Radio Jambo

Habari02 August 2022 - 02:18

Muhtasari


•Daniella alitoa wito kwa wanawake na wanamitandao wengine kusaidia kumwokoa Bi Sandra kutoka 'jela' aliyomo sasa.

•Daniella alidokeza kuwa Bi Sandra bado hajaweza kupata ujasiri wa kuzungumzia masaibu anayopitia  nyumbani.

Wiki iliyopita, moja ya habari zinazovuma zaidi kwenye mitandao ya kijamii nchini Uganda ni madai ya mwimbaji maarufu Weasel Manizo kumshambulia na kumdhulumu mkewe Sandra Teta.

Picha zilizomuonyesha Sandra akiwa amevimba na kuchubuka usoni zilisambazwa kote mitandaoni sambamba na uvumi kuwa anaendelea kupata afueni nyumbani baada ya kupigwa vibaya na mwanamuziki huyo.

"Mwimbaji Weasel anaripotiwa kumpiga mpenzi wake Sandra Teta. Kwa sasa anauguza majeraha," Ripoti ya kituo kimoja cha habari nchini Uganda ilisoma.

Bi Sandra hata hivyo alijitokeza kupuuzilia mbali madai ya kupigwa na mumewe na badala yake kudai  alikuwa ameshambuliwa na majambazi wakati akielekea nyumbani mnamo Julai 22, 2022 usiku.

"Kwa kurejelea picha zilizosambaa kwenye Vyombo vya Habari, nikiwa njiani kutoka kazini Ijumaa usiku, nilivamiwa na majambazi wasiojulikana ambao walikimbia na simu yangu, mkoba na Ush1.3M. Kwa muda wa wiki moja iliyopita nimekuwa kwenye matibabu na ninaendelea kupata nafuu," Teta alisema kupitia Instagram.

Weasel ambaye ni kakake Chameleone  aliunga mkono kauli ya mkewe na kubainisha kuwa alikuwa akipata afueni nyumbani.

Mkewe Chameleone, Daniella Atim, hata hivyo amesisitiza kuwa shemeji huyo wake ana tatizo na amekuwa akimnyanyasa mkewe kimwili.

Daniella  kupitia ukurasa wake wa Instagram alitoa ushahidi mpya kuhusu shambulio la awali la Weasel kwa mkewe. Alidokeza kuwa Bi Sandra bado hajaweza kupata ujasiri wa kuzungumzia masaibu anayopitia  nyumbani.

"Hizi ni picha za Sandra za mwezi Desemba ;Sandra anahitaji msaada wetu sote, kwa namna yoyote ile .Anahitaji sisi sote kupaza sauti zetu ili kumsaidia katika jambo la kwanza muhimu zaidi, kujiamini kwake. Sote tuweke uzito nyuma ya Sandra na tumsaidie kutembea safari hii," Daniella aliandika chini ya picha za kutia huruma za mkewe Weasel.

Katika picha hizo, Bi Sandra alionekana kuwa na michibuko mwili mzima ikiwa na pamoja na kwenye  shingo, mgongo, makwapa na magoti yake.

Daniella alitoa wito kwa wanawake na wanamitandao wengine kusaidia kumwokoa mwanasoshalaiti huyo wa Rwanda kutoka 'jela' aliyomo sasa.

"Watoto wa Sandra wanastahili bora zaidi!" Alisema.

Katika chapisho lingine, mkewe Chameleone alidokeza kuwa watoto wa shemejiye wanaumia sana kufuatia mzozo kati ya wazazi wao.

"Hawa ni watoto wa Sandra wakitupwa nje ya eneo lake la kazi. Kimila watoto hawa pia ni watoto wangu. Je, huwa tunasimama kwa sekunde moja na kufikiria jinsi tukio hili litakuwa na athari kwa watoto hawa wasio na hatia miaka 10-20 kutoka sasa?" Daniella aliandika chini ya picha zilizoonyesha watoto wa Weasel wakiwa wameachwa nje ya lango huku wakionekana wenye huzuni kubwa.

Daniella alitoa wito kwa Weasel kusaidiwa kupambana na hali inayomuathiri, Sandra kupata haki na watoto wao kulindwa .

Weasel na Bi Sandra  walianza kuchumbiana mwaka wa 2018 na tayari wako na watoto wawili pamoja.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved