logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+Picha) Ruto aiteka Nairobi mamia ya wafuasi wakifurika Nyayo

Azimio wamejumuika katika uwanja wa Kasarani weney uwezo wa kusheheni takribani watu elfu sitini huku Mrengo wa Kenya Kwanza ukiongozwa na DP Ruto ukikongamana uwanja wa Nyayo unaosheheni watu elfu 35.

image
na Radio Jambo

Habari06 August 2022 - 09:15

Muhtasari

• Ruto atafanya mkutano wake katika uwanja wa Nyayo huku Raila akiwa uwanja wa Kasarani.

Wafuasi wa Naibu Rais William Ruto katika uwanja wa Nyayo mnamo Agosti 6, 2022 Picha: WILFRED NYANGERESI

Baada ya miezi kadhaa ya kampeni za kutupiana maneno na cheche kali miongoni mwa wanasiasa, hatimaye kipindi hicho kinafikia kikomo leo kulingana na sheria za katiba kwamba kampeni zitamatishwe angalau siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu.

Miungano miwili hasimu Azimio la Umoja One Kenya na Kenya Kwanza imejiandaa vilivyo kuweka rekodi katika siku hii ya mwisho huku mirengo yote ikikongamana katika sehemu tofauti jijini Nairobi.

Azimio wamejumuika katika uwanja wa Kasarani weney uwezo wa kusheheni takribani watu elfu sitini huku Mrengo wa Kenya Kwanza ukiongozwa na DP Ruto ukikongamana uwanja wa Nyayo unaosheheni watu elfu 35.

Awali kulikuwepo na wasiwasi kuhusu uwezekano wa Ruto na Kenya Kwanza kupewa kibali cha kukongamana Nyayo ila Alhamisi mahakama ilitoa amri kwamba waruhusiwe kujumuika pale.

Hapa tunakuandalia baadhi ya picha za kufana kuonesha jinsi wafuasi wa Kenya Kwanza wamejitoma kwenye uwanja wa Nyayo.

Wafuasi wa Naibu Rais William Ruto katika uwanja wa Nyayo mnamo Agosti 6, 2022 Picha: WILFRED NYANGERESI
Wafuasi wa Naibu Rais William Ruto katika uwanja wa Nyayo mnamo Agosti 6, 2022 Picha: WILFRED NYANGERESI
Wafuasi wa Naibu Rais William Ruto katika uwanja wa Nyayo mnamo Agosti 6, 2022 Picha: WILFRED NYANGERESI
Wafuasi wa Naibu Rais William Ruto katika uwanja wa Nyayo mnamo Agosti 6, 2022 Picha: WILFRED NYANGERESI
Wafuasi wa Naibu Rais William Ruto katika uwanja wa Nyayo mnamo Agosti 6, 2022 Picha: WILFRED NYANGERESI
Wafuasi wa Naibu Rais William Ruto katika uwanja wa Nyayo mnamo Agosti 6, 2022 Picha: WILFRED NYANGERESI
Wafuasi wa Naibu Rais William Ruto katika uwanja wa Nyayo mnamo Agosti 6, 2022 Picha: WILFRED NYANGERESI
Wafuasi wa Naibu Rais William Ruto katika uwanja wa Nyayo mnamo Agosti 6, 2022 Picha: WILFRED NYANGERESI
Wafuasi wa Naibu Rais William Ruto katika uwanja wa Nyayo mnamo Agosti 6, 2022 Picha: WILFRED NYANGERESI

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7

logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved