logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Klabu ya Sporting Lisbon wanataka kumsajili christiano Ronaldo

"Mwanangu, kabla sijafa, nataka kukuona ukirudi Sporting." Mamake Ronaldo.

image
na Radio Jambo

Habari18 August 2022 - 04:56

Muhtasari


•Nyota huyo wa Mashetani Wekundu aliwaichezea klabu hiyo wa Ureno zamani kabla ya kujiunga na United akiwa kijana mwaka 2003.

•Kuanzia msimu huu, mchezaji huyo hajakuwa na ushirikiano poa na wakuu wa klabu ya United baada ya kuonyesha dalili ya kuhama klabu hiyo.

 

Manchester United imebanduliwa kutoka Champions League

Mshambuliajiwa Manchester United, Cristiano Ronaldo anatarajiwa kurejea Sporting Lisbon kwa uhamisho wa bure, klabu ambayo mama yake anataka kumuona akiiwakilisha tena kabla hajafariki.

Sporting Lisbon wameripotiwa kuiambia Manchester United kwamba watakuwa tayari kumsajili Cristiano Ronaldo - lakini kwa uhamisho wa bure tu.

Nyota huyo wa Mashetani Wekundu aliwaichezea klabu hiyo wa Ureno zamani kabla ya kujiunga na United akiwa kijana mwaka 2003.

Mama yake Ronaldo, amekuwa na ndoto ya kumuona mshindi huyo mara tano wa Ballon d'Or akichezea tena Estadio Jose Alvalade, aliwaimwambia kuwa "Mwanangu, kabla sijafa, nataka kukuona ukirudi Sporting."

Na sasa ndoto hiyo inaweza kutimia, kwani gazeti la Independent linadai kwamba Sporting wanataka kumsajili tena mshambulizi wao wa zamani, ambaye anatamani sana kuhama Manchester United msimu huu na kuendelea kucheza soka ya Ligi ya Mabingwa.

Kufikia sasa, wakala wa Ronaldo Jorge Mendes hajaweza kupata mwenye anayestahili na yuko tayari kulipa mishahara  ya mchezaji huyo ya ziada juu ya ada ya uhamisho.

Klabu ya Sporting wamewasiliana na wakuu wa Old Trafford kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37, wakitaka kumsajili kutoka kwa United iwapo watakatisha mkataba wake msimu huu.

Kuanzia msimu huu, mchezaji huyo hajakuwa na ushirikiano poa na wakuu wa klabu ya United baada ya kuonyesha dalili ya kuhama klabu hiyo.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved