logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pritty Vishy Asema Ata'cheat Kama Mpenzi Wake Madini Hawezi Kutekeleza Majukumu Yake

“Kama hawezi kutekeleza kazi yake mimi ndio ukweli nitachepuka kusema kweli, nitachepuka kama mtu hataki niondoke zangu nitachepuka," - pritty Vishy.

image
na Radio Jambo

Habari18 August 2022 - 12:38

Muhtasari


• “Mimi ni yule mtu ambaye kama anataka mahusiano yavunjike mimi niko tayari, kama hakuna mustakabali hakuna na kama mustakabali uko basi tuendelee,” Pritty Vishy

Msanii Madini Classic na mchumba wake Pritty Vishy katika hafla moja awali

Mtayarishaji wa maudhui Prityy Vishy kwa mara nyingine tena amezungumzia mahusiano yake mapya na mwanamuziki Madini Classic ambapo amedokeza kwamba yeye hataona tatizo kama mahusiano yao yatagonga mwamba kwani hawezi kubembeleza ili mambo yanyooke na atajipa shughuli tu bila kufikiria mara mbili.

“Mimi ni yule mtu ambaye kama anataka mahusiano yavunjike mimi niko tayari, kama hakuna mustakabali hakuna na kama mustakabali uko basi tuendelee,” Pritty Vishy alimuambia Dr. Ofweneke kwenye mahojiano katika kituo kimoja cha runinga humu nchini.

Pia mwanadada huyo mwenye misimamo isiyotetereka alisema kwamba yeye yuko tayari kabisa kuchepuka ikitokea Madini Classic hawezi kutekeleza majukumu yake katika nafasi yake kama mchumba wake.

“Kama hawezi kutekeleza kazi yake mimi ndio ukweli nitachepuka kusema kweli, nitachepuka kama mtu hataki niondoke zangu nitachepuka, nitamuonesha kwamba hii ni Nairobi na sikuja jana tu lakini kama itafanyikiwa basi tutaendelea na natarajia kuwa na familia na mtoto mmoja ni sawa juu ya hii uchumi,” Vishy alisema bila kupepesa macho.

Alisisitiza kwamba ukweli ni kwamba alichepuka dhidi ya mpenzi wake wa zamani Stivo Simple Boy kwa kile alisema kwamba mwanamuziki huyo wa Freshi Barida hakuwa anatekeleza majukuu yake kama mwanaume ndani ya nyumba na ndio maana akaamua kutoka nje ya mahusiano yao ili kukidhi mahitaji ya hisia za mwili wake.

Pritty Vishy walitengana na mchumba wake wa zamani Stivo Simple Boy na kuchafuana kwa matusi vikali mitandaoni huku kila mmoja akimkandia mwenzake kwa kutaka kujitakatisha.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved