logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hisia zangu kwa Harmonize zinaimarika kila siku- Kajala akiri

Wapenzi hao walirudiana mwezi Mei baada ya kutengana katika hali tatanishi Aprili mwaka jana.

image
na Radio Jambo

Habari21 August 2022 - 05:50

Muhtasari


•Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 39 sasa amekiri kuwa mapenzi yake kwa Harmonize yanaendelea kukua kadri siku zinavyosonga.

•Kwa sasa Kajala sio mchumbe wa Harmonize tu bali pia  ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya usimamizi ya Konde Music Worldwide

Takriban miezi mitatu baada yao kurudiana, wasanii wa Bongo Harmonize na Fridah Kajala Masanja wanaonekana kulifurahia sana huba lao.

Wapenzi hao walirudiana mwezi Mei mwaka huu baada ya kutengana katika hali tatanishi mnamo mwezi  Aprili mwaka jana.

Miezi mitano iliyopita Harmonize alimtema kipusa wa Australia aliyekuwa anachumbiana naye, Briana Jai, na kuanza juhudi za kufufua mahusiano yake na Kajala. Wakati huo alikiri kuwa hisia zake kwa Kajala bado zilikuwa hai.

"Kuhusu Briana sina Tatizo naye kabisa, yeye ni mtu mzuri ila hatuko pamoja, sababu moja  nilimwambia nimetengana na mtu bila kugomabana na nampenda sana sasa sina uhakika kama nimemove on lolote linaweza kutokea maana itakuwa ni kitendo kizalendo pia mimi kurudi nyumbani," Harmonize alisema kupitia Instagram mnamo mwezi Machi.

Kufuatia hatua hiyo alianza kuweka za mchwa kwa lengo la kumrejesha Kajala na hatimaye kufanikiwa takribani miezi miwili baadaye.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 39 sasa amekiri kuwa mapenzi yake kwa Harmonize yanaendelea kukua kadri siku zinavyosonga.

"Hisia zangu kwa mtu huyu zinaimarika zaidi na zaidi kila siku @harmonize_tz," Kajala alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe huo na picha zao pamoja wakielekea nchini  Burundi ambako Harmonize anatumbuiza wikendi hii.

Kwa sasa Kajala sio mchumbe wa Harmonize tu bali pia  ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya usimamizi ya Konde Music Worldwide.

Alianza rasmi kazi yake katika Konde Gang mapema mwezi uliopita baada ya mchumba wake kumteua kwa wadhifa huo mwezi Juni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved