logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Wavulana walikuwa wananicheka kuwa niko mnene na sura mbaya" - Kinuthia

“Wavulana walikuwa wananicheka sana kutokana na unene wangu na kuwa na sura mbaya, Sasa ninapendeza kuliko hata wapenzi wao, mipaka rafiki zangu,” Kinuthia aliandika.

image
na Radio Jambo

Habari27 August 2022 - 08:12

Muhtasari


•“Sasa ninapendeza kuliko hata wapenzi wao, mipaka rafiki zangu,” Kinuthia aliwarushia bomu la moto.

Mkuza maudhui Kelvin Kinuthia enzi za utoto wake

Mkuza maudhui kupitia mtandao wa TikTok kwa kuvalia kama mwanamke, Kinuthia amepakia video moja mtandaoni humo ikiwa na picha yake moja ya zamani enzi za utoto wake.

Katika picha hiyo ambayo mtoto Kinuthia amevalia sare ya shule maridadi kabisa, amesema kwamba wavulana walikuwa wanamcheka na kumkebehi kwamba alikuwa na sura isiyovutia hata kidogo.

Kinuthia anasema kwamba vijana wa kiume enzi hizo za utoto wake walikuwa wanamkejeli sana kutokana na umbile lake la unene wa kibonge hivi na pia kwamba sura yake ilikuwa mbaya, tofauti na sasa ambapo anawachanganya wanaume wasijue kama ni mwanaume kweli ama ni mwanamke anayejificha katika jinsia ya kiume ila uvaaji wa kike.

“Wavulana walikuwa wananicheka sana kutokana na unene wangu na kuwa na sura mbaya,” Kinuthia aliandika.

Kinutjia katika klipu hiyo ambayo ameambatanisha picha ya zamani na sasa, aliendelea kusema kwamba licha ya hao vijana kumcheka na kumkejeli, lakini sasa mitikasi yake kwenye mitandao ya kijamii kwa uvaaji na kujipodoa kama mwanamke kamili kumempa umaarufu na utajiri mkubwa kuliko hata wachumba wa wavulana hao.

“Sasa ninapendeza kuliko hata wapenzi wao, mipaka rafiki zangu,” Kinuthia aliwarushia bomu la moto.

Kwa muda mrefu Kinuthia amekuwa akikatalia kuzungumzia kuhusu mrengo wake wa suala zima la kimapenzi huku kwa kipindi kimoja katika mahojiano ya simu na watangazaji alifoka na kukata simu alipoulizwa msimamo wake katika tasnia ya mapenzi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved