logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Abiria mwingine afariki ndani ya ndege ya Kenya Airways

Ndege hiyo ilikuwa ikielekea New York kutoka Nairobi.

image
na Radio Jambo

Michezo02 September 2022 - 13:12

Muhtasari


•Kifo hicho kilithibitishwa na shirika hilo siku ya Ijumaa kupitia taarifa.

•Ndege hiyo ilikuwa ikielekea New York kutoka Nairobi.

Abiria mmoja ameripotiwa kufariki ndani ya ndege ya shirika la Kenya Airways.

Kifo hicho kilithibitishwa na shirika hilo siku ya Ijumaa kupitia taarifa.

"Baada ya uchunguzi zaidi, wahudumu wa afya waliokuwemo ndani ya ndege hiyo walithibitisha kuwa abiria huyo ameaga dunia," ilisema taarifa hiyo.

Ndege hiyo ilikuwa ikielekea New York kutoka Nairobi.

Huyu ni abiria wa pili kuripotiwa kufariki kwa ndani ya ndege ya KQ katika muda wa wiki mbili.

Shirika hilo, almaarufu KQ, lilisema abiria huyo ambaye jina lake halikutajwa aliaga dunia mnamo Septemba 2, 2022 mwendo wa saa kumi na mbili unusu asubuhi.

Kisa hicho kilitokea ndani ya ndege ya KQ002.

Abiria aliyefariki wiki jana ndani ya ndege moja ya shirika hilo ambayo ilikuwa ikitoka New York hadi Nairobi alikuwa raia wa nchi mbili, Marekani na Kenya.

Mamlaka zilimtambua kama Peterson Njuguna Mwangi mwenye umri wa miaka 66 kutoka Lewisburg, Pennsylvania.

Ndege hiyo ya KQ ilitakiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) saa mwendo wa saa nne na dakika 32 asubuhi ya Jumatatu, Agosti 22 lakini kutokana na kisa hicho na matokeo yake kubadilishwa njia, ilitua Nairobi dakika chache baada ya saa moja usiku.

Dharura ya kimatibabu iliwalazimu marubani wa ndege kuelekeza ndege hiyo hadi Casablanca, Morocco.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved