Ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni!
Huku dunia ikizidi kuomboleza kifo cha malkia Elizabeth wa pili kutoka Uingereza, watumizi wa mtandao wa Twitter wameibua Tweet ya mganga mmoja hatari aliyebashiri kifo cha Malkia Elizabeth mwaka mmoja uliopita.
Mganga huyo kupitia Twitter yake amejieleza katika utambulisho wake kwamba yeye ni mtaalamu katika kutoa ubashiri kutumia ushirikina, voodoo.
Malkia alifariki Septemba 8 na Tweet ya huyo mganga kwa jina Orunmila inaonesha kwamab alipiga ramli na kutoa ubashiri wake kuhusu kifo cha Malkia kwamba kingetokea tarehe kama hiyo.
Ubashiri wake unaonekana kwenye Tweeter kutolewa mnamo Agosti 24 mwaka jana.
Baada ya ubashiri huo kutimia kwa kifo cha malkia, sasa Orunmila ametanua kifua na kutamba kwamba kama wewe uko hapo na bado huamini katika uganga wa vood basi umetupa mbao.
“Malkia wa Uingereza atafariki dunia tarehe 8 Septemba. Mimi naona tarehe hii ikimzingira juu ya kichwa chake. Wewe endeleea kutoamini katika voodoo na utaona,” mganga huyo aliandika mwaka jana Agosti kwa lugha ya Kifaransa.
La reine d'Angleterre va mourir le 8 Septembre je vois cette date planer au dessus d'elle, continuez à ne pas croire au vaudou vous verrez
— Orunmila (@orunmilavd) August 24, 2021
Jana baada ya ubashiri wake kugonga ndipo, mshirikina huyo alirudi kweney Twitter na kujisifu kwamba kazi yake ya voodoo si ya kubahatisha kwani huwa anabashiri na tofauti huwa ni kidogo sana. Alisema kwamab katika ubashiri wake mwaka jana, hangeweza kubashiri sahihi muda na chanzo cha kifo cha malkia Elizabeth.
“Hatuwezi kutenda au kushawishi, kutabiri tu, kujua mapema na wakati mwingine tofuati kidogo kizuri yaa makosa. Hapo sikuweza kujua saa wala sababu ya kifo,” mganga Orunmila aliandika.
Swali ni je, wewe huwa unaamini katika uganga wa kupiga ramli?