logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jinsi askari alivyopanga utekaji nyara wa mtu katikati mwa jiji la Nairobi - Polisi

Polisi huyo alikuwa ameshirikiana na watuhumiwa wengine watatu kumteka nyara daktari mmoja katika barabara ya Uhuru Hingway kabla ya kushikwa.

image
na Radio Jambo

Habari26 September 2022 - 07:48

Muhtasari


• Ripoti ya polisi ilisema watekaji wanne, miongoni mwao polisi walikuwa wamemteka nyara daktari mmoja katika barabara ya Uhuru.

Majarida mbali mbali ya humu nchini yamesimulia mtiririko wa matukio ya ukakasi jinsi polisi mmoja anayehudumu kati kati mwa jiji la Nairobi alishiriki katika kisa cha utekaji nyara wa daktari mmoja.

Poisi huyo mtuhumiwa David Balesa wa utekaji nyara aliviziwa na kukamatwa na maafisa waliokuwa wakiweka ulizni kwenye majengo ya bunge kwa tuhuma ya kufanya jaribio la kumteka nyara daktari mmoja kwa jina Nelson Mango.

Bw Balesa alinaswa pamoja na wengine watatu waliotambuliwa kama Silas Omach Omondi ambaye ni dereva wa Uber, Diana Cheruto Bungei na Hillary Kiprono.

Watuhumiwa hao wa utekaji walifnya kitendo hicho katika barabara ya Uhuru Highway.

“Iliripotiwa na mtawala mkuu mwendo wa saa kumi na mbili jioni kwamba kulikuwa na mtu Dkt Nelson Rading Mango ambaye alitekwa nyara na watu wasiojulikana kando ya Barabara Kuu ya Uhuru kuelekea Barabara ya Bunyala. Ndipo maafisa wa polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Bunge walikimbilia eneo la tukio,” ripoti ya polisi ilisomeka kwa sehemu.

Baada ya ripoti hiyo kuzunguzwa kwa maafisa wote wa polisi, wane hao waliviziwa wakiwa pamoja na mtu huyo ambaye alitajwa kuwa daktari.

Baada ya kuwavamia, Mango alifanikiwa kutoroka kutoka kizuizi cha watekaji nyara na polisi pia wanamsaka ili kuandikisha taarifa.

Watuhumiwa waliokamatwa watashtakiwa kwa makosa ya kujifanya, kutoa taarifa za uongo na kumiliki pingu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved