logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+video) Mwanadada alia kuachiwa bili ya chakula na mpenzi mzungu, "Alijilipia yake pekee"

"Kukutana mara ya kwanza na mpenzi wako mzungu na anavuta kalamu kutoka mfukoni na kuanza kupiga hesabu ya bili yake" - Aliandika.

image
na Radio Jambo

Habari27 September 2022 - 07:43

Muhtasari


• Alivuta kalamu kutoka mfukoni na kuanza kupiga hesabu ya bili yake na kuacha ingine yenye wewe ulikula,” mwanadada alieleza.

Mwanamke mmoja kwenye mtandao wa Tiktok amewachekesha wengi baada ya kuelezea masaibu aliyopitia wakati wa mtoko na mpenzi wake mwenye asili ya kizungu.

Mwanadada huyo alielezea kwamba ilikuwa ndio mara ya kwanza wanakutana na mpenzi huyo wake Mzungu ambapo waliingia katika mgahawa kushtaki njaa na kilichotokea baada ya chakula ni kumbukumbu za matukio ambayo ataenda kaburini akiwa anayakumbuka.

Katika video aliyoipakia, alieleza kwamba baada ya mlo, mpenzi wake mzungu aliingia mfukoni na kutoa kalamu kuanza kupiga hesabu. Mzungu alipiga hesabu ya bili yote na kumtaka binti wa watu washirikiane kulipa ile bili pasu kwa pasu; kati kati!

“Tafakari kwamba upo katika kukutana mara ya kwanza na mpenzi wako mzungu na anavuta kalamu kutoka mfukoni na kuanza kupiga hesabu ya bili yake na kuacha ingine yenye wewe ulikula,” mwanadada mtumizi wa Tiktok alieleza kwa masikitiko makubwa kwenye klipu hiyo huku matukio yakionekana jinsi mzungu alitafuta program ya kikokotoo kwenye simu na kuhakikisha hesabu haimpigi chenga.

Watu mbali mbali walitolea maoni yao ya jinsi walijipata katika visa kama hivyo huku wengine wakisema mwanadada huyo alikuwa mpole mno, kwani angezua tafrani hapo hapo.

“Kusema ukweli dadangu wewe ni mkarimu, ingekuwa ni mimi hapo hapangekalika kabisaa,” mtumizi mmoja wa Tiktok alisema.

“Date yangu ya kwanza alisema tugawanye kulipa bili, nilimwambia hakuna haja, nikaingia mfukoni nikalipa bili yote na kuitisha kinywaji aina ya Champaigne juu. Nilimuamrisha kuondoka kwa sababu nilitaka kusherehekea mwanaume mwingine asiye na hela,” mwanadada kwa jina Anabela Pinote alisimulia.

“Nimepitia hii hapo awali. Nilishtuka na kuona aibu. Na hata aliniomba €5+ alikuwa na ujasiri wa kuniomba kwa kukutana mara ya pili,” Marilyn Raphael alifunguka pia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved