logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanaume akamatwa kwa kumbaka mama mjamzito hadi kufa

Mwanaume huyo alivizia nyumbani kwa marehemu wakati mume wake aliondoka kutazama pambano la ngumi.

image
na Radio Jambo

Dakia-udaku28 September 2022 - 13:19

Muhtasari


• Mtuhumiwa alikamatwa na kupatikana na baadhi ya vitu vya marehemu kama simu na nguo.

Mwanamke mjamzito

Kuna visa, mikasa, vioja na matukio ambao huokea mpaka wakati mwingine mtu utadhani si binadamu anakitekeleza bali shetani mwenyewe katika ngozi ya ubinadamu.

 

Ni kisa cha kusikitisha na ambacho kimegonga vichwa vya habari katika ukanda wa Afrika mashariki baada ya mwanaume mmoja kudaiwa kumbaka mwanamke mjamzito hadi kufa.

 

Mwanaume huyo kwa jina Mohamed Mwanjali ambaye ni mkaazi katika mkoa wa Iringa nchini Tanzania anashikiliwa na polisi nchini humo baada ya kudaiwa kuvizia familia moja usiku na kumbaka mwanamke aliyekuwa mjamzito hadi kusababisha kifo chake.

 

Kulingana na taarifa zilizochapishwa na mwanahabari maarufu Millard Ayo, Mwanjali alivizia nyumbani kwa mwanamke huyo usiku baada ya mumewe kutoka kuenda kutazama pambano ya ngumi baina ya mabondia ya Tanzania waliokuwa wakimenyana wikendi iliyopita.

 

Mwenyekiti wa Mtaa wa Maweni, Yassin Kisogole alinukuliwa na taarifa hiyo ya Ayo akisema Mwanamke marehemu  alitendewa ukatili huo usiku wa kuamkia September 25,2022 wakati Mumewe akiwa Mtaa wa jirani alipokwenda kushuhudia pambano la ndondi la Mandonga vs Abeid na kisha lile la mwisho usiku huo lililowakutanisha mabondia Twaha Kiduku vs Abdo kupitia.

Mapambano hayo yalikuwa yanapeperushwa moja kwa moja kwenye runinga.

 

Mume wa marehemu aliporudi nyumbani baada ya kumalizikqa kwa  mapambano hayo ya ngumi, alipofika mlangoni alikuta mlango upo wazi wakati akiingia ndani alimuona Mtuhumiwa akitoka katika moja ya chumba na kukimbia ndipo alipojaribu kumkimbiza bila mafanikio.

 

Alipoingia ndani alimkuta Mtoto wa Marehemu mwenye umri wa miaka mitano ambaye alimmsimulia kuwa kulikuwepo na mtu aliyevizia nyumbani humo na kumziba mama yake mdomo kabla ya kumuangusha chini na kumtendea kitendo hicho cha unyama.

 

Baada ya taarifa hizo Mume huyo wa Marehemu alienda kutoa taarifa Polisi, ambapo Mtuhumiwa alikamatwa na Polisi nyumbani kwake ambako alikutwa na baadhi ya vitu vya Marehemu ikiwamo simu ya mkononi na nguo ambazo alizichukua mara baada ya kutekeleza tukio hilo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved